Kuna siri gani ambayo Jenerali Venance Mabeyo anataka kumpa Rais Samia Suluhu?

Kwa watu wanaopenda kutafakari mambo kwa kina si rahisi kupuuzia hizi kauli mbili zilizotolewa na pande mbili tofauti lakini zenye mlengo unaofanana wa "kujizuia kusema jambo fulani"

Kiongozi wa juu kabisa wa mambo ya usalama anafahamu umuhimu wa mbeba taarifa ya siri! Anafahamu kabisa kuwa mtu mwenye taarifa ya siri anawindwa na kundi lisilotaka siri yao ivuje

Taarifa ya Siri inayopelekwa kwa Rais mwenyewe maana yake hiyo ni "classified information" imevuka level ya "top secret"

Aliyesema hivyo anafahamu kabisa kuwa kwa kusema "nina classified information" ni kuhatarisha usalama wa pande zote mbili yaani kama wanashindwa kumpata mwenye hiyo classified information watamuwinda anayekusudiwa kufikishiwa hiyo taarifa!

Unaweza kujiuliza, CDF alishindwa nini kujizuia kutamka "kuna dokezo" muhimu lakini naomba nisiseme hapa nitakuona ofisini.

Kwanini asiende moja kwa moja ofisini? Kwanini aliliweka kwenye hutuba yake??

Kama hiyo haitoshi familia wakati wanatoa neno la shukurani wakasema Hayati Rais Magufuri kabla hajaaga dunia aliomba mambo matatu kwa Mungu lakini kati ya hayo matatu wameweza kukumbuka mawili tu!!..na jambo la tatu "wote" waliokuwepo "wamelisahau"!

Inawezekanaje hiii?? Kati ya vitatu, penye watu zaidi ya watatu wote wakumbuke vitu viwili tu vinavyofanana??

Hapa pia ukitafakari kwa upana "ni kama kuna jambo" wameona lisiende hewani kwa maslahi fulani ambayo huenda busara imewatuma si vizuri umma ukajulishwa kwa sasa

Pamoja na busara hiyo, inaonekana kwa makusudi kabisa CDF na Familia wameamua wawafikishie watanzania ujumbe fulani kwa lugha ya fasihi!

Si rahisi watu wengi wote kwa pamoja kusahau jambo moja na kukumbuka mawili yanayofanana!

Wangesema wakati anataja la tatu kabla hajalimaliza "roho yake ikatwaliwa" hapa inaeleweka lakini si kulisema halafu waliokuwepo wote walisahau kwa pamoja...huu ni muujiza pia!

Ni kazi kwa wabobevu wa uchambuzi kutatua kitendawili kilichoachwa na CDF pamoja na famalia ya marehemu kwa pamoja!

Raha ya milele umpe Eee Bwana, apumzike kwa Amani!
 
Umewaza kama nikivyowaza.. I'm sure Hayati alijua fika kuwa umauti unaenda kumfika na ninahakika ilo dokezo ambalo Mabeyo kalisema aliambiwa na JPM mwenyewe na ndo siri waliyoificha Familia.
 
I
Labda kawaombea msamaha waliomfanyia mabaya
 
Binafsi nadhani kaweka tu tension,kuna ile kibiblia wanasema astahiliye hofu mpe hofu....kuna ujumbe umelengwa kwa watu fulani.
 
Ni hivi, Samia Suluhu Hassan siyo Kaimu rais bali rais (Kamili na halali kwa vigezo vyote) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hivyo asiwepo wa kuwa na matarajio ya eti marehemu aliagiza hiki au kile.
Hivyo basi, Samia Suluhu Hassan hayupo pale kuingozwa na kivuli cha Magufuli.
Zama za Magufu ndiyo zimeshapita.
 

System ndo SUPREME. MKUU wao ... oversight organs zote ni CDF!

Ni kina nani walijaribu kutikisa kiberiti na baba lao ni yupi, na kwa hiyo kwa kumtumikia nani? Kama kinacho kula ki nguoni, UMUHIMU wa kufahamisha UMMA adui zrtu ni NANI ni muhimu
 
Soma katiba ibara ya 37 yote kisha jikite zaidi kifungu cha 10.....utapata majibu kuwa your wish is unrealistic....
 
haya sasa mama D, mama la mama katika ubora wake.
 
Military diplomacy naiyona kuwapa kichefuchefu wanaoimezea mate Tanzania. Nikiitafakari na kuona ilikuwa muhimu sana kwa Mkuu wa majeshi kusema maneno yale. Kongole kwake aliyeona inafaa kwa Mh CDF aseme neno whatsoever kinachoongelewa kwa yeye kusimamia.

Waheshimiwa Wana diplomasia, Nchi katika @regimechange huwa ni wakati sensitive sana hasa katika ulimwengu wa mataifa yanayonusa nchi yenye neema na ukawa na udhaifu eneo flan flan.

Nimpongeze Mh Samia Hassan na kumuombea mema, lakini isitoshe kusema alale mahala pema Mh Rais Marehemu JPM. Mh Samia ana kila sababu ya kufanya mabadiliko katika safu ya uongozi kutokana na teuzi zilizofanywa na Hayati ama zilizotokana na mapenzi binafsi. Nikitoka mfano kwa aliyeweka korona cha dorali chumbani kwake haya ni matumizi mabaya ya madarasa.
 
Bado najiuliza kile kitu ambacho CDF Mabeyo aliahidi kwenda kumwambia mama ofisini kwake ni nini hass? Je ni hiyo habari ya utoroshwaji wa madini pamoja na kuwepo na ukuta pamoja na ulinzi wa jeshi kule mirerani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…