Kuna siri gani ya mafanikio ya ghafla kwa wafanyabiashara ya kuuza smartphones?

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Wengi huwa ni vijana wadogo tu wapo kwenye 20s hasa wahitimu wa degree na diploma.

ni tabaka tofauti na wauza simu wengine, wao hujitofautisha kwa kuuza simu zenye brand zinazotrend ulaya na marekani tu kama iphone, samsung na google pixel... Simu za kichina na vitochi hawauzi.

Simu hizo bei huwa zimechangamka kwahio wengi wapo kwenye majiji yenye watu wenye vipato vya juu wanaoweza zimudu kama Dar (maduka yao yamejaa Makumbusho, Mwenge na kariakoo), Mwanza, Arusha.

kwa macho yangu nimeweza kuwa observe kwa miaka kama miwili hawa vijana na nimeona wengi biashara imebadili maisha yao ghafla.

  • vijana wanaonekana smart sana, wanatupia pamba na hawapo nyuma kwenye fashion.
  • kwenye usafiri nako si haba, kijana mwenye 20s kumiliki crown, subaru, bmw yupo juu huyo.
  • kwakuwa wanazijua simu na wanazifatilia, wengi wanamiliki simu za gharama za kisasa
  • kwenye sekta ya kula bata, hawana shughuli ndogo, uwanja huu wanafanya kweli japo kwa level za kibongo.
  • wanaishi sehemu smart, wapo waliopanga apartment nzuri, wapo waliopanga nyumba nzima, n.k huku wakiendelea na ujenzi
  • ni ngumu sana kugombaniana mwanamke, binti mwenye simu ya kichina ya laki 2 iliyochoka anahongwa hata iphone ya laki 5 yenye wateja wachache, binti kapewa tu hio iphone ashazuzuka bila kujali ya mwaka gani
 
Kama unajua bottom line ya biashara zao au mitikasi yao..achana nao...kila mtu ale mkate wake
 
unawazungumzia wale vijana wa makumbusho wenywe mindevu ?? kuna mtu aliuziuwa iphone 11 kumbe ndani ni mashine ya xr [emoji16][emoji16]
 
Vipi huwa mitaji wanatolea wapi?
 
Mie naona hizi biashara za simu ni kama kazi ya ziada au kuficha chanzo kikuu cha income yao. Ila ni kweli hawa vijana wanaonekana smart sana na inaonekana wana mkwanja mrefu na usafiri mzuri. ila nakua siamini kama hiyo biashara ya simu pekee ndiyo inawatoa. Kuna kitu nyuma ya pazia
 
hizi simu kwa jumla wanachukulia wapi
Hizi simu zipo dubai, ulaya au china na zinakuja kama used as new au certified refurbished. Kwa hiyo ukinunua kwa jumla bei inakuwa ndogo. Ukija kuuza kwa bei elekezi inakuja na faida nzuri. Kwa hiyo hawa wanachuo hutumika kama madalali kupata wateja kuliko kukaa na simu dukani.
 
Changamoto ya hizo simu nyingi zinarudishwa na wateja, hivyo uwe aware na hilo.
Maana katika piece 10 utakazouza zitakazoenda kulalamikiwa na wateja na hatimaye kuja kubadilisha ni 50/50
So wengine wanavumilia wengine inabidi ubebe lawama wengine uwabadilishie.
Matatizo ni mengi kwakweli.
Nipo kwa hii field so nafahamu risk zake na changamoto tunakutana nazo sokoni
 
Hehehe wamefikiwa na kwa uchache wao. Nobody understands kwanini hawa vijana wana hela hivi😂😂😂
 
huo utafiti labda umeufanya kwa wauza simu wa mchongo, ni nadra sana mtu karudisha simu mbovu kwenye duka alilonunua labda wawe wapiga dili. binafsi hadi sasa nishanunua simu zaidi ya 10 zikiwemo efurbished 3 na hakuna hata moja nimewahi kurudisha.
 
Exactly
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…