Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unakutana na duka Lina cover za simu protector chaji na simu kadhaa lakini muuzaji kapanga nyumba ya 200k ,ana crown na simu Kali .Mie naona hizi biashara za simu ni kama kazi ya ziada au kuficha chanzo kikuu cha income yao. Ila ni kweli hawa vijana wanaonekana smart sana na inaonekana wana mkwanja mrefu na usafiri mzuri. ila nakua siamini kama hiyo biashara ya simu pekee ndiyo inawatoa. Kuna kitu nyuma ya pazia
Wengi huwa ni vijana wadogo tu wapo kwenye 20s hasa wahitimu wa degree na diploma.
ni tabaka tofauti na wauza simu wengine, wao hujitofautisha kwa kuuza simu zenye brand zinazotrend ulaya na marekani tu kama iphone, samsung na google pixel... Simu za kichina na vitochi hawauzi.
Simu hizo bei huwa zimechangamka kwahio wengi wapo kwenye majiji yenye watu wenye vipato vya juu wanaoweza zimudu kama Dar (maduka yao yamejaa Makumbusho, Mwenge na kariakoo), Mwanza, Arusha.
kwa macho yangu nimeweza kuwa observe kwa miaka kama miwili hawa vijana na nimeona wengi biashara imebadili maisha yao ghafla.
- vijana wanaonekana smart sana, wanatupia pamba na hawapo nyuma kwenye fashion.
- kwenye usafiri nako si haba, kijana mwenye 20s kumiliki crown, subaru, bmw yupo juu huyo.
- kwakuwa wanazijua simu na wanazifatilia, wengi wanamiliki simu za gharama za kisasa
- kwenye sekta ya kula bata, hawana shughuli ndogo, uwanja huu wanafanya kweli japo kwa level za kibongo.
- wanaishi sehemu smart, wapo waliopanga apartment nzuri, wapo waliopanga nyumba nzima, n.k huku wakiendelea na ujenzi
- ni ngumu sana kugombaniana mwanamke, binti mwenye simu ya kichina ya laki 2 iliyochoka anahongwa hata iphone ya laki 5 yenye wateja wachache, binti kapewa tu hio iphone ashazuzuka bila kujali ya mwaka gani