Kuna tatizo gani NIDA?

Kuna tatizo gani NIDA?

Hoaxer

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2022
Posts
2,726
Reaction score
6,852
Naomba mniulizie kwa mtendaji mkuu wa NIDA Kibaha mkoa wa Pwani.

Kwanini inachukua zaidi ya mwezi kupata namba (sio kitambulisho) katika ofisi ya Kibaha?

Tunaomba mkuu wa mkoa aingilie kati.
 
Mkubwa hivyo ilikuwaje hata namba tu huna?
Wakati wenzako tunapambania kombe ulikuwa wapi?
2020/2021/2022 ni miaka ya watoto under 21 kufatilia hizo mambo.

BTW pole.
 
Naomba mniulizie kwa mtendaji mkuu wa NIDA Kibaha mkoa wa Pwani.

Kwanini inachukua zaidi ya mwezi kupata namba (sio kitambulisho) katika ofisi ya Kibaha?

Tunaomba mkuu wa mkoa aingilie kati.
Hakuna shida kamilisha Taratibu....NIDA wanajitaidi sana wanafanya kazi usiku na Mchana
Tunapaswa kuwapa pongezi sana wanafanya kazi katika mazingira magumu sana
DG wa NIDA na Timu yako pongezi sana kwa kazi zuri
 
Mhhhhhhh oooooooohhh uzembe ni uzembe kabisa uwezekano wa kumaliza vitambulisho vyote watafanya kazi gani wanajitahidi kuwa wazembe ili waendane na kasi ya serikali na kwakuwa sisi wananchi hatujawahi kupata kitu bila kuhangaikia masiku mengi kila siku kila taasisi inarudi kwenye mazoea yao
 
Kibaha pamezidi, Kuna foleni hata Sasa hivi lkn wakifika watatoka wote halafu watarudi saa nne, saa sita wanatoka wote mpaka saa nane. Bosi yupo, mkuu wa wilaya yupo, mkuu wa mkoa yupo.
Sisi hatutaki hivyo vitambulisho, watupe namba tu. Vitambulisho watakwangulia vocha. Halafu msiwaruhusu wafanyakazi wa NIDA kuchati na simu zao wakati wa kazi.
Mkuu wa nida muondoe huyu bosi wa nida pwani. Tuletee mtu anayejua wsjibu wake.
 
Naomba mniulizie kwa mtendaji mkuu wa NIDA Kibaha mkoa wa Pwani.

Kwanini inachukua zaidi ya mwezi kupata namba (sio kitambulisho) katika ofisi ya Kibaha?

Tunaomba mkuu wa mkoa aingilie kati.
Nilifika kuchukua kitambulisho changu mtumishi akanikabidhi box la vitambulisho nitafute mwenyewe kisha akasepa!
 
NIDA MTAISABABISHIA NCHI HASARA KUBWA SANA,
PINDI LAINI ZISIZOHAKIKIWA ZITAKAPOZIMWA KILIO KIKUBWA NI NIDA,HII NI KWASABABU WENGI WATAKAOZIMIWA LAINI NI WALE WALIOTUMIA VITAMBULISHO AMBAVYO SIO VYAO.MNA MLOLONGO MREFU SANA MTU NI MTANZANIA KWANINI KUNAKUA NA USUMBUFU KUPATA KITAMBULISHO?SUBIRI MUONE ANGUKO LA UCHUMI KWA ASILIMIA KADHAA.
 
Back
Top Bottom