Ki ukweli ifike wakati binadamu tuache unyanyapaa. Kikubwa ni kujiridhisha kile anachokuambia kina ukweli. Siku zote huwa nasema upendo wa kweli ndo kila kitu. Kama kuoa mke mwenye watoto basi atukuwa anapasha kiporo je wale wote wanaoolewa na wanachepuke wana tofauti gani.
Binafsi naamini hakuna mwanamke chini ya jua anayependa kuwa single mother lkn ni matokeo tu katika safari ya mapenzi. Kweli kuna wengine wanasababisha wao kujishikisha mimba ili wawin mapenzi wanaishia kutelekezwa lakink kuna wengine wanadanganywa na wanaodanganya ni wanaume haohao ambao wanapaza sauti kusema usioe single maza.
Nina ushuhuda mmoja nina sister wangu mmoja ktk safari yake alikutana na mwanaume wakapendana maisha yakaenda,,,sababu alishamuaminisha baadae sister akapata ujauzito baada ya kupata ujauzito yule akaja kugundua kuwa ni mume wa mtu na walikuwa na mgogoro na mke na wametengana. Sister akaamua kumpiga chini jamaaa akasema siwezi kuwa na mwanaume muongo na asiye muaminifu. Basi bwana akarudi kwa mkewe sister akahangaika mwenyewe na mtoto hadi alipofika drs la pili. Akapata mwanaume akamuoa kwa ndoa kabisa.
Lkn ikumbukwe yule jamaa aliyezaa naye walikata mawasiliano kabisa hakujali kuna mtoto wala nini na sister wala hakumtafuta na wakati huo sister alikuwa anafanya biashara tu ya kuuza machungwa ili alee mtoto wake.
Baada ya kuoana na huyo bwana wakabahatika kupata watoto wengine watatu,,,mwanzo yule bwana aliyemuoa akawa anamtemga kiaina mtoto wa sister japokuwa mahitaji ya msingi alikuwa anatimiza ila vipaumbele vya luxury alikuwa anatoa kwa watoto wake. Basi dada kugundua hilo akawa anamwambia mwanangu usihuzunike hata kama anakutenga wewe kazana kusoma baba yako yupo lkn hajali chochote hivyo shukuru Mungu hata kwa mahitaji ya msingi unayopata ukikazana kusoma na ukiwa mtoto mwema atakupenda tu basi dogo akawa anashika wosia wa maza ake. Dogo akawa kichwa darasn in anaongoza,,,mwanzo mwisho. Kufika sekondary hivyohivyo. Asa alipofika chuo baba yake wa kambo ndo akashtuka akaanza kuonyesha mapenzi akajua huyu ndo wa kwanza anaweza kuja kufanikiwa akalea wadogo zake.
Baada ya kufika chuo dingi wake akamtafuta sister akamwambia ooh namtaka mtoto aje nimpe urithi wake mara ooh ajuane na ndugu zake. Dada akamshirikisha mume wake ,,,bahati nzuri mume wake akampa ushirikiano akasema mtoto ameshakuwa mkubwa mwambie mwenyewe. Basi wakamuita mtoto wakamwambia baba yako anakuhitaji uende ukajuane na ndugu zako mtoto alichowajibu kuwa huyu aliyenilea toka nikiwa mdogo ndiyo baba yangu,,,kama kweli alikuwa ananipenda angenitafuta siku zote hizo.
Hivyo hadi leo dogo yupo anamaisha yake alimaliza chuo akapata kazi nzuri analea wadogo zake baba yake wa kambo anakula bata.
Siku zote ukitaka kufanya jambo fanya kwa moyo mmoja usifanye kwa mashaka,,,hata mtoto mdogo ukimionesha upendo atarudisha upendo,,,changamoto sisi binadamu masimango na kauli mbaya.