Kuna tatizo lolote kupenda vitabu 'vinavyohubiri' mafanikio?

Kuna tatizo lolote kupenda vitabu 'vinavyohubiri' mafanikio?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Kwa sasa kumekuwa na mlipuko mkubwa wa kusoma vitabu hivi vya mafanikio na miongozo binafsi(self-help books). Usomaji wowote ule ni mzuri kuliko kutosoma kabisa. Hivyo usomaji wa vitabu hivi ni jambo zuri. Lakini ni kama mlipuko hivi, kila kona kila site kila sehemu watu wanazungumzia vitabu hivi. How to, Laws of...nk.

Nafananisha usomaji huu na ujio wa Injili ya mafanikio na uponyaji. Watu wamekimbia kusikiliza mahubiri yanayohubiri kuacha dhambi, utu wema, ucha Mungu nk na kukimbilia mahubiri yanayosema juu ya kupata pesa, nyumba, kuolewa, watoto na kupona magonjwa. Yaani yanayohubiri wanayotaka wao wasikie. Au ni wamekuwa practical, wakitaka mahubiri yanayotatua shida zao za sasa? Na wachungaji wa kisasa wamegundua hilo na wanapiga pesa nyingi. Mahubiri hayo badala ya yale magumu yanaathari zozote kwa muumini?

Binafsi sivipendi hivi vitabu, lakini najiuliza pengine ni chuki zangu tu na vina faida kubwa sana ambazo nakosa.

Usomaji wa vitabu hivi vya mafanikio binafsi badala ya vile traditional vyenye maudhui mbalimbali, yanaathari zozote kwa msomaji? Na faida zake zipi?
 
Back
Top Bottom