Kuna tatizo uongozi wa mwendokasi (BRT)

Kuna tatizo uongozi wa mwendokasi (BRT)

maroon7

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
11,311
Reaction score
15,640
Wakuu tunaomba mjitahidi kutoa huduma inayoeleweka. Sijui ni nani anaepanga route za magari maana imagine mtu unakaa kituoni lisaa lizima gari zinapita chache mno na zimejaa hakuna hata pa kusimama.

Mtu unaamua uende hadi terminal ya kivukoni au gerezani unakuta hali ndio haifai. Jitahidi kuamrisha magari yaondoke maana unakuta yamepaki tu na watu wanasubiri huduma. Kuna wakati mnajitahidi ila mda mwingi kunakua hakuna coordination nzuri.
Hebu angalia hizi picha na ni mchana tu saa nane saizi hali ni hivi.

Kama tatizo lingekua uchache wa magari basi tusinge experience hii shida muda wa mchana. Lakini imekua kinyume chake yaani mchana hali inakua mbaya zaidi.

Kama kuna tatizo ombeni serikali ichukue hatua au hadi wawachukulie nyie hatua?

IMG_20230104_135000.jpg
IMG_20230104_135009.jpg
IMG_20230104_135017.jpg
 
hakuna kitu kibaya kama ku copy na ku paste , waliiga vya ulaya wanashindwa na kuiga usimamizi, kimsingi mradi ni mzuri sana ila usimamizi wa kueleweka haupo, na kikubwa zaidi hawana MABASI ya kutosha, kama wangekuwa na uwezo kila baada ya muda kadhaa ngoma inaingia kituoni bongo ingekua kama mbele tu ila sasa mabasi yamechokaaaa yale yale ya zamani mengi mabovuuuuu kwa kweli msaada unahitajika pale
 
Ukitaka kujua Dar na huu mradi jinsi gani hauna mazingira mazuri nenda Gerezani mida ya jioni kwenye kituo cha mwendokasi , yaani foleni ya kufa mtu hadi unajiuliza hawa wanafika kwaao muda gani na mpaka wengine wamekaa chini kwenye mstari kutokana na uchovu wa kupanga foleni kwa muda mrefu.

Gari likija watu nyomi hata sehemu ya kupumua ni shida watu wanabanana sana ,kuna mdau humu alitoa wazo hela za mwendokasi bora zingejengwa treni za kisasa kupita sehemu mbalimbali za jiji ambalo behewa moja lingechukua abiria wengi zaidi kuliko sasa na kuondosha foleni na kusave pesa.
 
hakuna kitu kibaya kama ku copy na ku paste , waliiga vya ulaya wanashindwa na kuiga usimamizi, kimsingi mradi ni mzuri sana ila usimamizi wa kueleweka haupo, na kikubwa zaidi hawana MABASI ya kutosha, kama wangekuwa na uwezo kila baada ya muda kadhaa ngoma inaingia kituoni bongo ingekua kama mbele tu ila sasa mabasi yamechokaaaa yale yale ya zamani mengi mabovuuuuu kwa kweli msaada unahitajika pale
Mabasi yapo mengi ila coordination yao ni mbovu. Maana tatizo lingekua uchache wa mabasi tusingepata shida hiyo mida ya mchana.
 
Dar raha sana isingekuwa kukimbia ile kesi yangu ya kumkata mtu makalio na panga nisingehamia huku kipumbwe
 
Wakuu tunaomba mjitahidi kutoa huduma inayoeleweka. Sijui ni nani anaepanga route za magari maana imagine mtu unakaa kituoni lisaa lizima gari zinapita chache mno na zimejaa hakuna hata pa kusimama.

Mtu unaamua uende hadi terminal ya kivukoni au gerezani unakuta hali ndio haifai. Jitahidi kuamrisha magari yaondoke maana unakuta yamepaki tu na watu wanasubiri huduma. Kuna wakati mnajitahidi ila mda mwingi kunakua hakuna coordination nzuri.
Hebu angalia hizi picha na ni mchana tu saa nane saizi hali ni hivi.

Kama tatizo lingekua uchache wa magari basi tusinge experience hii shida muda wa mchana. Lakini imekua kinyume chake yaani mchana hali inakua mbaya zaidi.

Kama kuna tatizo ombeni serikali ichukue hatua au hadi wawachukulie nyie hatua?

View attachment 2468757View attachment 2468758View attachment 2468759
Hawa wangekuwa na railway system kwa ajili ya mwendokasi ingekuwa poa sana maana ni low maintenance na haina blah blah kama hii mwendokasi ya sasa. Sijui hiyo kampuni iliyopata tenda ya kusimamia italetaje suluhisho la kudumu wakati miundombinu si rafiki
 
Nahisi kwa jinsi mazingira yetu yalivyo,train ingekua headache zaidi maana ikiondoka usubiri irudi.. Hata zikiwa mbili zinapishana bado ingekua shida sana ukizingatia mavituo yenyewe yapo jirani, kwa mtazamo wangu mabasi nadhani ni sawa ila usimamizi ndio sio poa
 
Back
Top Bottom