Kwani hawalipwi mishahara yao? Wanalalamika ofisi haziendi kwani ni za kwao? Huo uzalendo wa kutaka kazi za serikaki ziende vizuri wameupata lini na kwasababu zipi?
Sio hawa tuliokuwa hatuwakuti ofisini saa nne asubuhi? Sio hawa waliokuwa wanashughulikia mambo yetu mwaka mzima bila majibu?
Waambie kama mwenye ofisi anakulipa unachostahili ila kazi zake anazichelewesha mwenyewe muache aue ofisi yake kwani wa kuulizwa ni yeye sio wewe.
Saa nyingine muwaambie hao mnaowaita watumishi waache kiherehere na umbea, wewe ni daktar mfano dawa hakuna na umeshamwambia mwenye nchi yake hataki kuleta dawa, nenda kazini mwisho wa mwezi kachukue chako acha umbea, ukiulizwa waambie wamuulize aliyewaahidi na sio wewe.
Wanaolalamika ni wezi tu, mtu anabomoa nyumba yake kwa hiari yake wewe uliyekodishwa kufabya jazi ya kubomoa unalia nini wakati unalipwa hela ya kubomolea?
Kama magar ya ofis hayatembei kwani daladala nazo hazitembei na wao wanalazimishwa kutembea kwa miguu? Magar gani hayo hayatembei? Yale wanayoyatumia kwenye harusi zao na mambo yao? Wewe ni secretary ulikuwa unakuja kwa daladala unawashwa nini ukiona mashangingi yamepakiwa uwani? Kama ulipewa gari kama mkataba wako unavyosema na wamekupokonya bila kukupa usafiri nenda kashtaki kuvunjiwa mkataba wa kazi wakulipe.
Waambie hao watumishi waache unafiki kama wanatendewa mabaya wanashindwa vipi kuungana kuishtaki hii serikali choka mbaya wanawaambia nyinyi wa vijiweni wakati hamuwezi kuwasaidia chochote.