Kuna tija gani kuingiza mchepuko wa BRT phase 3 airport?

GANJIBHAAI

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2018
Posts
790
Reaction score
2,049
Pamoja na takwa la Serikali la kuhakikisha miundo mbinu inasomana, Kwa maoni yangu, sioni tija ya mradi wa BRT awamu ya tatu kuingiza mchepuko wake ndani ya Airport ya Kimataifa ya Julius Nyerere kutokana na sababu chache zifuatazo:
  1. Ukizingatia umbali wa vituo vingine vya BRT kituo cha airport karibu na puma, kingine kituo cha BRT Karakata (almost mita 500)
  2. Matumizi bora ya ardhi airport ni sehemu nyeti sana na finyu kwa kwa maana ya JNIA lazima tuwe makini ya kuchagua nini tunajenga na kwa nini?
  3. Ongezeko la traffic jam kuingia na kutoka airport kwa maana ya distance ya barabara kubwa T24 eneo ni finyu la plus mabasi ya BRT totally chaos……….
 
Sio lazima kila mtu ajue kwamba wewe ni mjinga. Ungeweza kujizuia kutoandika huu uzi ili kuficha ujinga wako. Inaonekana wewe kupanda ndege ni jambo nyeti sana na kusahau kabisa ni usafiri kama usafiri mwingine. Watu wanapanda ndege na kwenda kupanda zao daladala au bodaboda kiroho safi kabisa.
 
Mbona Reli ingefaa zaidi eneo hilo.

Mabas airport? Bad idea.
 
Kama kawaida yako; kumbe upumbavu unatokana na jina lako na huyo unaye mwita mama.
Kwa hiyo unatueleza kuwa wewe umepanda ndege. Huyo unayemsema hapa ni wapi kazungumzia swala la kupanda ndege?
 
Umetoka nje ya mada kiongozi hebu soma uzi wangu vizuri.
 
Kama kawaida yako; kumbe upumbavu unatokana na jina lako na huyo unaye mwita mama.
Kwa hiyo unatueleza kuwa wewe umepanda ndege. Huyo unayemsema hapa ni wapi kazungumzia swala la kupanda ndege?
Hakuna siku nimeandika comment humu halafu asijitokeze mwendawazimu kupinga na kutoa lugha chafu. Hongera sana kwa kuwa mwendawazimu wa kwanza kwenye huu uzi.
 
Mkuu, ungekaa kimya tu.
 
Ulivyoandika mchepuko nikadhani demu.

adriz de mbusii
 
Hakuna sehemu Nchi hii watu wanapigwa hela ndefu kama hapo Airport, kuanzia Bolt Hadi Tax hela ni ndefu Sana, kama huna usafiri binafsi Pana shida Sana hapo. Hata kwa wageni wanaokuja kutoka nje kama kipato chake si kikubwa ni lazima atalalamika.

Pia huwezi kumtoa MTU na mabegi aende Hadi puma kule, imagine Bibi Mzee na mibegi yake anafikaje kule? Na ukitaka amkodi MTU Hadi puma ni Yale Yale Tu hujamsaidia.
 
Kwa kweli Mkuu umetisha na kutokuwa na ufahamu. Unauliza tija ya kupeleka BRT airport? Umewahi kusafiri kwa ndege, ukawa mjini na kupanda Bolt na kukutana na foleni njiani hadi uka-miss ndege yako? Sasa jibu la hiyo changamoto ni BRT toka mjini kwenda airport
 
Watu wengi hawana exposure, kwa MTU yoyote ambaye katumia Airport yetu mara kadhaa anaweza akaona uhitaji wa public transport maeneo hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…