Kuna tofauti gani kati ya funzo adhabu na laana?.

FYATU

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2011
Posts
5,882
Reaction score
5,087
Kuna wakati kwenye maisha Mtu unakutana na mitihani mpaka unajaribu kujiuliza kama hiyo ni adhabu ya makosa uliyowahi kufanya, au ni funzo tu unapitia baada ya kutoka kwenye mstari au la ni laana ya Mtu au Watu uliowakosea kwenye harakati zako za maisha.

Sasa mtihani unabaki namna ya kutambua kile unachopitia ni nini haswa.

Ni kwa namna gani basi Mtu unaweza kubainisha kuwa hii ni adhabu au ni mafunzo napata au ni laana ya Mtu/watu?.
 
Kwa nini usiishi tu kwa kuangalia leo haikuwa siku nzuri kesho nitajitahidi kuifanya iwe nzuri. Kuliko kuwaza mambo ya laana na adhabu. Hayo mara nyingi huwa ni mawazo ya mtu ku justify mambo aliyoyafanya au kufanyiwa kwa nini usi own mistake zako na kujipanga vizuri kuliko kusingizia adhabu na laana
 
Vipi kama makosa hayo umemtendea Mtu mwingine na kumsababishia athari? Je unafikiri mambo yatabaki tu kama kawaida?.Au basi ni nini wajibu wa Binadamu mmoja kwa mwingine?.
 
Vipi kama makosa hayo umemtendea Mtu mwingine na kumsababishia athari? Je unafikiri mambo yatabaki tu kama kawaida?.Au basi ni nini wajibu wa Binadamu mmoja kwa mwingine?.
 
Vipi kama makosa hayo umemtendea Mtu mwingine na kumsababishia athari? Je unafikiri mambo yatabaki tu kama kawaida?.Au basi ni nini wajibu wa Binadamu mmoja kwa mwingine?.
Karma, cause and effect kwamba kila unalofanya lazima utalipwa unahisi hizi sheria zina apply duniani, sababu kuna watu wanafanya mambo mabaya na wanapesa nyingi ila maskini siku zote kila akifanya kosa kidogo analipwa unahisi ni fair au dunia haipo kama tunavyofikiria
 
Huu nao ni mjadala mwingine na niliwahi kutaka kuanzisha uzi wake.Kwa kifupi ni kwa nini tunadhani kuwa na pesa ni kipimo cha utimilifu wa Mtu?.Mimi sidhani kama ipo hivyo ila ninachojua kumdhulumu Mtu mwingine haki yake kamwe mambo hayawezi kubaki vilevile,iwe ni haki ya kuishi,kufurahia maisha n.k.
 
kitu kikubwa na hatari ni njaa na ugonjwa, achana na hayo upweke sijui huna mke/mme au mtoto. Na mtu mwenye pesa anaweza ku afford hivyo. Usilinganishe mtu ambaye anakula anachotaka, akiumwa ana hela za kujitibu ila kakosa ndoa au mtoto et ni sawa na mtu anaye lala njaa au yupo nyumbani hana hela ya kutibu ugonjwa
 
Ni kweli fedha ni muhimu sana kwa sababu inahusika katika mahitaji yote ya binadamu.

Hatahivyo, fedha si alama inayomaanisha kwamba utajiri si kutokuwa masikini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…