Kuna tofauti kati ya wafuasi na wanachama

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
WAFUASI na WANACHAMA
..POLISI WANAFANYA KAZI NZURI

Kuna tofauti kati ya wafuasi na wanachama.

Bwana Yesu alikuwa na wafuasi (disciples). Kanisa lina wanachama (members) na wafuasi wachache.

Kazi ya Kanisa ni kubadilisha wanachama kuwa wafuasi. Kazi ya shetani ni kubadilisha wafuasi kuwa wanachama wa Kanisa.

Vyama vya siasa vina wafuasi na wanachama. Kazi ya kila siku ya vyama ni kubadilisha wanachama wawe wafuasi.

Kwa namna ya pekee, jeshi la Polisi limejitolea kufanya kazi tukufu ya kushughulika na wafuasi na wanachama wa vyama. Kazi hii wanaifanya ifuatavyo:

1. Kwa vyama vya Upinzani, Polisi wanawabadili wanachama kuwa wafuasi. Kwa hiyo wanachama katika vyama vya Upinzani wanapungua lakini wafuasi wanaongezeka. Hii ni Kazi ya kizalendo. Pongezi sana mtani.

2. Kwa chama tawala cha CCM, Polisi wanawabadili wafuasi kuwa wanachama. Kwa hiyo wafuasi wa CCM wanapungua lakini wanachama wake wanaongezeka. Hii pia ni kazi ya kizalendo. Pongezi sana mtani.

Kazi ambayo ingefanywa kwa gharama kubwa na vyama vya siasa inafanywa kwa utukufu na jeshi letu la Polisi.

Haya ni maoni yangu..
Kamanda Siro ana maoni yake na ukiyakataa anakukung'uta..
Msomaji una yako...

Huu ni ukurasa wa maoni.


Askofu Bagonza
 
Msomaji una yako...
Huu ni ukurasa wa maoni.
Asante kwa bandiko elimishi, mimi maoni yangu ni kutoa tuu ushauri. Kwa vile IGP Kamanda Sirro emesema Jeshi la Polisi lina ushahidi, nadhani ni busara tungesubiria kuusikia huo ushahidi.

Nashauri tujenge utamaduni wa kuheshimu maoni ya wengine hata kama hatukubaliani nayo.

P.
 
Kumbuka kesi za kubambikia 147 zilizofutwa. Kumbuka kesi ya Viongozi wa Chadema iliyofutwa na Serikali kutakiwa kurudisha 350 million kwa Chadema. IGP ni muongo sana.
 
Kwani CHADEMA wamesema/tangaza wanakwenda kukataa maoni ya SIRRO mahakamani watakapohudhuria kiongozi wao akifikishwa Mahakamani?
 
MUNGU AMLINDE Baba Askofu Bagonza..
 
Reactions: BAK
Tatizo ni pale ushahidi ukikosekana hulipwi fidia ya usumbufu kama mashekh wa uamsho
 
mara nyigi nilikuwa najiuliza kwa nini viongozi na wafuasi wa Chadema mara zote ni Wakorofi na huioa lugha za kuitisha mamlaka?
Kumbe Jibu lake ndio hili, kweli waswahili husema mtoto wa nyoka ni nyoka.
Kumbe kiongozi wa Chama alikuwa ananunua na kupanga vitendo vya kigaidi....ndio maaana wafuasi wa chadema ni wakorofi hatari.
Ushauri wangu, viongozi wa Chadema na wafuasi wote badilikeni, acheni vitendo vya uvunjifu wa amani, na kwa sasa IGP katangaza operesheni kubwa ya kuwasaka wale wote wenye lengo la kuvunja sheria.
Ushauri kwa Jeshi la polisi;
kuna haja ya kufuatilia nyendo za viongozi na wafuasi wa Chaema kila kona ya nchi.
 
Hawa wapuuzi huwa wanataka kila mtu afuate matakwa yao! Asante kwa ushauri mwanana siyo kama wa Benson oh! Nimwite Askofu Bagonza
 
Maoni ya 1+1=3 katika normal/natural mathematics hayatasikilizwa. Wewe utakuwa Mjing ambaye unahitaji kuelimishwa na si kusikilizwa utoe muhadhara wa hesabu. Labda katika matrimonial mathematics, hiyo hesbu itasikilizwa na kujadiliwa.

Kuna majina yamekosewa, angalia uwezekano my friend. Ulikuwa mwanaharakati wa haki za binadamu, njaa , Mayalla ikakugeuza.
 
yeyote atakaye thubutu kutoa pua yake eti kwenda mahakamani atachakazwa.
tena tunaomba Jeshi letu lisisubirie wafike au wakaribie maeneo ya mahakama wanapaswa wachakazwe kabla hata hawajatoka majumbani kwao.
 
Tatizo lako na wengi wa CCM ni mawazo kuwa Rais ni "Mungu". Mnashau kuwa Rais ni mtumishi wenu, ameajiliwa na wewe. As long as una thinking kma hiyo lazima uona mtu kutaka haki itendeke anaitisha serikali. Serikali ni mtumishi wako and not otherwise. Ukiwa na akili za kujua hivyo, basi hutaandika "mavi" kama hayo uliyoandika.
 
yeyote atakaye thubutu kutoa pua yake eti kwenda mahakamani atachakazwa.
tena tunaomba Jeshi letu lisisubirie wafike au wakaribie maeneo ya mahakama wanapaswa wachakazwe kabla hata hawajatoka majumbani kwao.
Mbona baba yako na maa yako ni wenzetu tutakuwa na o mahakamani? watachakazwa vile vile
 
kama baadhi ya wafuasi wa Chadema wanavyo fikiri kuwa Mbowe ni malaika. jambo usilo lijua ni usiku wa giza.
ngoja kesi ianze kusikilizwa ndipo utakapo ujua uovu na umafia wa Mbowe.
acha ushabiki.
 
Mbona baba yako na maa yako ni wenzetu tutakuwa na o mahakamani? watachakazwa vile vile
hata mke wake tu hana mawazo wala mpango wa kwenda mahakamani sasa wewe nn kinakuwasha? hebu tuliza hapo nyumbani.
 
kama baadhi ya wafuasi wa Chadema wanavyo fikiri kuwa Mbowe ni malaika. jambo usilo lijua ni usiku wa giza.
ngoja kesi ianze kusikilizwa ndipo utakapo ujua uovu na umafia wa Mbowe.
acha ushabiki.
Nilidhani naongea na literate man kumbe ni lumpen proletariat, kwaheri! Na kwa vile siyo size yangu, telling it from your post, I am blocking you to reduce the number of lumpen to respond to!
 
Nilidhani naongea na literate man kumbe ni lumpen proletariat, kwaheri! Na kwa vile siyo size yangu, telling it from your post, I am blocking you to reduce the number of lumpen to respond to!
Hizi shift za product ya mikesha ya mwenge kwa kweli zinatuharibia jamvi...akitoka Jumbe Brown, anaingia zandrano, akitoka zandrano anaingia Idugunde, akitoka Idugunde anaingia Kamanda Asiyechoka and the list goes on...

Kwa kweli kodi zetu zinatumika hovyo kweli kweli kwa kuyafuga haya matakataka...yaani mwenge umeharibu nchi! Na hapo bado Etwege na Elitwege
 
Huna akili masikini !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…