BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
WAFUASI na WANACHAMA
..POLISI WANAFANYA KAZI NZURI
Kuna tofauti kati ya wafuasi na wanachama.
Bwana Yesu alikuwa na wafuasi (disciples). Kanisa lina wanachama (members) na wafuasi wachache.
Kazi ya Kanisa ni kubadilisha wanachama kuwa wafuasi. Kazi ya shetani ni kubadilisha wafuasi kuwa wanachama wa Kanisa.
Vyama vya siasa vina wafuasi na wanachama. Kazi ya kila siku ya vyama ni kubadilisha wanachama wawe wafuasi.
Kwa namna ya pekee, jeshi la Polisi limejitolea kufanya kazi tukufu ya kushughulika na wafuasi na wanachama wa vyama. Kazi hii wanaifanya ifuatavyo:
1. Kwa vyama vya Upinzani, Polisi wanawabadili wanachama kuwa wafuasi. Kwa hiyo wanachama katika vyama vya Upinzani wanapungua lakini wafuasi wanaongezeka. Hii ni Kazi ya kizalendo. Pongezi sana mtani.
2. Kwa chama tawala cha CCM, Polisi wanawabadili wafuasi kuwa wanachama. Kwa hiyo wafuasi wa CCM wanapungua lakini wanachama wake wanaongezeka. Hii pia ni kazi ya kizalendo. Pongezi sana mtani.
Kazi ambayo ingefanywa kwa gharama kubwa na vyama vya siasa inafanywa kwa utukufu na jeshi letu la Polisi.
Haya ni maoni yangu..
Kamanda Siro ana maoni yake na ukiyakataa anakukung'uta..
Msomaji una yako...
Huu ni ukurasa wa maoni.
Askofu Bagonza