Kuna tofauti kubwa ya uchekeshaji na ufanyaji ujinga Idris Sultan ni mfanya ujinga sio mchekeshaji

Iliuchekeshe walau kichekesho chako kiwe na mambo makuu mawili.

1. Ukweli ( tazama joti na mpoki) wana igiza ukweli lakini uwasilishwaji wake ndio unacheka.

2. Maumivu ( mpoki) huyu bwana anatabia ya kusema maumivu ya watu.

Jee, idris yeye amafit wapi?
 
Niliangalia comedy ya mnaijeria Klint de drunk,j amaa anachekesha sana,kuna clip moja kachekesha weeee,alipokuwa anamalizia akasema "nimejitahidi kuchekesha ila kama hujacheka basi tatizo lako ni kubwa mno lipo juu ya uwezo wangu",watu wakajikuta wamecheka,comedy ni kipaji huwezi kuforce,kuna watu sura zao ni comedy mbali na kuongea,akiongeza na vichekesho ndo unacheka.Ila hawa sasa wa kuforce vipaji ndo shida
 
Bongo wachekeshaji wa ukweli ni watatu tu

Marehemu Max
Mzee Majuto
Mpoki

walobaki ujinga mtupu.
 
Bongo tuna uhaba wa wachekeshaji sana
 
Huyo mzee Majuto mi hanichekeshagi kabisaa ki ukweli. Idris kuna mambo yake yananichekesha. Anyway we differ


Majuto hata mimi hanichekeshi hata kidogo na Idris pia wangu Jotiii Masanja mama Emma (Wakuvanga) pale tuu anapokuwa mama Emma na sauti ya kinyaki
 
Jemutaiii... MAMITOOO... Nomaa sanaa!!
 
Unachosema ni kweli,kuna kichekesho cha joti anajiita malkia wa instagram ile ameongea ukweli kbs,maisha wanayoishi wadada wengi wa Inst ni uhalisia ni tofauti kbs
 
Kikundi cha uchekeshaji kizuri Tanzania ni KASH KASH GROUP

Wachekeshaji mmoja mmoja mzuri ni

1) Majuto

2) Joti

3) Sumaku

4) Mpoki

5) Brother K

Wengine hakuna kitu.
 
Hahaahaa kitaaa kulikuwa na ule mchezo wa matani yaani hatari sana. Unaambiwa ulikunywa suda ukapanda chupa mara uliambiwa useme kirefu cha BP ukasema barkenja na paulo
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Anaforce Kuwa Stand Up Comedian!Hawezi Fika Level Za Omondi
Hajachelewa kama ana puncline atafute watu wamuandikie. Tatizo ninaloliona wabongo wengi wanafikiri kuimprovise ndiyo kuwa mchekeshaji mzuri au muigizaji mzuri. Wengi huwa hawajiandai au wanajiandaa kijuujuu.
Hata mzee majuto kuna maneno anatoa unajua hili limemjia tu wala hakujiandaa na unakuta anatoa neno hata siyo fun. Ukitoa kichekesho cha papo hapo hakikisha ni kichekesho kweli, usibweteke kuwa mimi kila neno mikisema watacheka tu.

Napendaga sana kumuangalia MCA tricky. Anavyotoa story lazima ucheke. Na niwachache sana wanaweza toa story ya kuchekesha wengi hudokoadokoa bila kuwa na story yenye mtiririko. Huyu Idrissa akijibiidiisha kwenye kuandika,research na hata kutafuta wanaojua wamuandikie anaweza fanikiwa.
 
Umenena vyema
 
na wadada wengi wanao mfollow [emoji3][emoji23][emoji23] wanajichekesha wapate attention kutoka kwake
 
+ bakila, mkude
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…