Pamoja na kwamba, mwananchi ndio mjenga nchi, lakini kwa uelewa wangu mdogo, naona kwa Tanzania mambo ya tozo yamezidi.
Ni bora serikali iwaambie ukweli wananchi kwamba, nchi inaelekea kufilisika ili tuanze kujifunga mkanda, kuanzia viongozi mpaka wananchi.
Kinachoendelea sasa Tanzania ni unyonyaji, yaani wananchi tunakamuliwa lakini viongozi waandamizi wa serikali wao wanaendelea kula bata kwa tozo zetu. Hii inasikitisha sana.
Hizi tozo ni ishara ya kwamba, serikali haina vyanzo vikubwa vya mapato zaidi ya tozo za wananchi, na kama vipo basi havitoshelezi kuendesha nchi kwa sasa kama vile kulipa madeni ya nje na kutekeleza shughuli za maendeleo ndani ya nchi.
Hali hii imepelekea kuanzishwa utitiri wa tozo ili angalau kuleta ahueni kwa serikali.
Ikumbukwe, miaka mitano nyuma kuna mikopo ilikopwa kwa fujo na ilitakiwa kuanza kulipwa baada ya miaka mitano, nahisi ndio muda wa kulipa umefika.
Cha ajabu, pamoja na hali ngumu, lakini tunaona viongozi waandamizi wa serikali (mawaziri, wakurugenzi, mameneja nk), wenyewe hawapo tayari kujifunga mkanda, bali wanaendelea kuponda mali za wananchi. Haingii akilini serikali kutumia zaidi ya bilioni 500 kununua magari ya kifahari ya viongozi kila mwaka, kwani wakinunua land cruiser za kawaida kuna ubaya gani? Hapo ndio unagundua Tanzania tunahubiri uzalendo bila vitendo.
Nilikuwa nahisi, vyanzo vya uhakika na vya muda mrefu vya mapato ya serikali ni kuhakikisha tunauza bidhaa au huduma nje ya nchi ili tupate fedha za kigeni na uchumi ukue. Kwa mfano, tuna ardhi ya kilimo kuzalisha mbegu za mafuta ya kupikia, pamba kwa ajili ya nguo, tumbaku, madini, mbuga za wanyama nk.
Lakini kujikita katika tozo, ni dalili mbaya kwa nchi yenye rasilimali za kila aina.
Halafu hizi tozo mbona ni kama vile zinakatwa katika vyanzo vilevile, yaani mzunguko wa pesa ni ule ule wa ndani?. Tutaendelea kweli kwa staili hii, au ndio kuumiza wananchi?
Hebu tujiulize, kwa mfano, mtumishi wa serikali analipa kodi (paye) katika mshahara wake, halafu akienda kutoa hela mara ya kwanza anakatwa tozo, akitoa mara ya pili anakatwa tena tozo. Hii itapelekea mtumishi atoea hela nyingi kwa pamoja na kuziweka ndani, na benk kuishiwa hela. Ni suala la muda tu.
Wahindi ndio hawataweka hela tena benki.
Serikali waambieni ukweli kama nchi imefilisika, msione aibu. Tuangalie wapi tumejikwaa na tuanze upya wananchi na viongozi.