Binafsi ni mshabiki wa mpira wa kiwango cha kati, siyo shabiki lialia anayeweza kulia timu yake ikifungwa.
Sasa nilikuwa nawauliza mashabiki lialia wa Yanga, je, kuna ubaya wowote Feisal kwenda Azam kutafuta hela ili ajenge future yake?
Ikumbukwe, mashabiki walikuwa wanasema Feisal ana kiwango cha kwenda nje ya nchi, lakini mpaka anakubali kwenda Azam ina maana ameishajikatia tamaa ya kwenda nje, hivyo anataka kutengeneza pesa kupitia Azam ili awekeze mana umri nao unaenda!
Hebu tujiulize, hivi Feisal hata akibaki Yanga, je, ataweza kung'ara, kupata namba ya uhakika na pesa nyingi kwa miaka mitatu ijayo? Binafsi kwa maisha ya soka yalivyo, naona kabisa Feisal pale Yanga atapata changamoto za wachezaji wazuri na hivyo kutokuonekana lulu ndani ya miaka mitatu ijayo.
Hivyo, tunavyokuwa tunamsakama Feisal, tufahamu kuwa na yeye anatafuta ridhiki ya maisha yake ya baadae.
Maisha ya mpira kwa sasa ni kutafuta pesa na siyo mapenzi na timu kama zamani!
Sent from my TECNO F1 using
JamiiForums mobile app