Kuna ubaya wowote Feisal kwenda Azam kutafuta hela ili ajenge kesho yake?

Hivi mashabiki wa yanga mchezaji wao akitaka kuhamia timu nyingine Tanzania ndio wanakumbuka alitakiwa kupata timu ya nje
 
Taratibu zikifuatwa Hamna matata.
 
Hii timu ya wacheza kigodoro ina watu wenye elements za kichawi,wanambania dogo asitengeneze future yake.
 
Hakuna aende tu,hata wanayanga hawamtaki pengo limezibwa.muhimu kwake kuangalia mkataba Yuko sahihi awaite akina jemedari,oruma na Geoff mbele vipaza sauti asaini Azam.kama mkataba unambana awaambie Azam aongee na Yanga mpira biashara,ila awape angalizo kuwa wasiingilie maslahi yake kuwalipa Yanga anacheza kwa ajili ya pesa sio kurahisha mtu.isije lingana na maboresho ya Yanga.
Ukiona amesaini Azam na anawatumikia alikuwa sawa kimkataba.na ukiona anazurura zurura kuwa na mashaka mkataba unambana mshauri aongee na Azam faster wakalipe kule jangwani.viongozi wanapenda ila mashabiki watampa wakati mgumu hasa akikosea uwanjani aondoke
 
Nimeandika kama shabiki wa Yanga wa kiwango cha kati, siyo shabiki ambaye yupo tayari kufa kwa ajili ya timu!

Nimeandika kwa ajili ya kuwashauri wana Yanga wenzangu na Watanzania wengine wabadilike, wajue kwamba, mpira ni biashara na waache kumtisha Feisal mpaka mama yake.

Kwani hujawaona hao wazee wa Yanga wanaitisha press conference na kupiga mkwara wa kususia bidhaa za Azam! Hizo ni dalili mbaya za ushabiki!

Hivi unahisi Feisal akiondoka Yanga pengo lake halizibiki kweli? Kwa wachezaji wote hao?

Yeye mwenyewe kaona kabisa ndani ya misimu miwili ijayo hawezi kucheza dakika 90 zote, ndo maana kaona ni bora apige hela za Azam kabla thamani haijashuka.

Tumuache Feisal apige hela za Azam atengeneze Future yake!



Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
hakuna ubaya kabisa fei kwenda kokote kule ila afate taratibu tu
 
hakuna ubaya kabisa fei kwenda kokote kule ila afate taratibu tu
Na akifuata utaratibu, basi wasimbanie mana wabongo tunajuana.

Akifuata utaratibu, utashangaa mtia saini wa barua ya uhamisho haonekani ofisini, wala hapatikani kwenye simu mpaka dirisha la usajili linafungwa!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Hivi unafuatilia tetesi za mchezaji bora chopukizi wa kombe la dunia 2022 Enzo ?

Ukifuatilia ndio utajua Azam wamekosea wapi?Japo walifanya kwa siri ila walichofanya ni uhuni.

Kila mchezaji mkataba wake unaweza kuvunjwa haijalishi ana miaka mingapi kwenye mkataba wake na hiyo timu cha msingi ni kufuata utaratibu na si kutumia njia zisizo sahihi kumfuata mchezaji na kumshawishi bila kupitia kwenye timu ambayo anamkataba nayo wakati hujawasilisha maombi kwa barua kwa timu yenye mkataba nae.

Liverpool wanamtaka Enzo,walichofanya kuwaface Benifica kwa Barua kwamba tunamtaka Enzo now wapo kwenye negotiation.So Liverpool kama angetaka kufanya uhuni hasinge shindwa kwani hela anayo na Liverpool ni timu kubwa na yenye historia kubwa ila kaamua kufuata taratibu zilizoweka na FIFA.

Hamna anayemzuia Fei kuondoka anaweza kuondoka ila taratibu zifuate na hata ukiandika barua unaweza ukakubaliwa au ukakataliwa na mchezaji akaondoka free mkataba wake ukiisha kama ikivyokuwa kwa Flamini na Pogba.

Cha msingi taratibu zifuate tusifanye mambo kihuni sababu tu unafedha basi hufuagi taratibu.

Madrid ni timu tajiri duniani, ila kwa CR7 seven walifuata taratibu zote na kaa ukijua Madrid ilikuwa timu ya ndoto yake CR7 na bado alifuata taratibu zote na hakugomea mazoezi sababu bado alikuwa chini ya mkataba wa Man Utd.

Tuwe professional na si kuendesha mambo kihuni sababu tu una hela.
 
vinginevyo fei hatacheza pipote pale
 
Katika hali halisi sio mbaya lakini hakuna shabiki atakaefurahia kuona mchezaji mzuri anaondoka kwenye timu anayoishabikia ila yote kwa yote hata feisal mwenyewe hajatumia maamuzi ya busara kuondoka kwa namna alivyofanya
 
Kwa ishu ya Feisal Yanga wameonyeaha ukomavu, waswahili wanasema Kuku wako kwanini uhangaike ku mkimbiza wakati Jioni atarudi Bandani!! [emoji3][emoji3]
 
Hakuna ubaya kabisa; na anaweza hata kuamua kuwa hataki kucheza mpira ila anataka ajishughulishe na shughuli nyingine. Tatizo ni kuwa anatakiwa afuate utaratibu. Kazi nyingi za mikataba huwa siyo za kuacha kwa utashi kwa vile mwajiri huwa ameweka matumaini kwa mwajiriwa kuwa atatkeleza majukumuyake ipasavyo wakati wa mktaba. Najua kwa Marekani waalimu pia husaini mikataba kuwa hawawezi kuacha kazi kiholela kabla mkataba wake haujaisha kwa sababu anakuwa amepangiwa masomo ambayo huenda ni yeye tu ndiye mtaalam wa somo alilopewa kwa hiyo akiondoka kunakuwa na ugumu wa kupata mtu mwingine wa kujaza pengo lake wakati watoto hawafundishwi.
 
Kwenye mkataba ukishaweka release clause hakuna haja ya hayo mabarua, na anayelipa hela ya ku triger release clause mara nyingi ni mchezaji mwenyewe sio timu inayomtaka, refer sakata la Neymar, ndio kama la feisal
 
Kwenye mkataba ukishaweka release clause hakuna haja ya hayo mabarua, na anayelipa hela ya ku triger release clause mara nyingi ni mchezaji mwenyewe sio timu inayomtaka, refer sakata la Neymar, ndio kama la feisal
Hamna kitu kama hiko hii sheria imetungwa hasa kuzilinda timu zisizokuwa na nguvu kiuchumi.

As long mkataba mmeingia watu wawili hata wakati wakuvunjwa lazima pande zote ziliziane.
 
Ni kweli kuwa mpira ni biashara,
Swala je, kama amevunja mkataba kisheria na yupo huru kutokana na udhaifu wa mkataba nini kina mzuia kujiunga na Timu nyingine? Yanga wanawezaje kumzuia mchezaji huru?
Timu nyingine zinapataje kigugumizi Cha kumsajili mchezaji huru?


Sent from my Redmi Note 8 Pro using JamiiForums mobile app
 
Hamna kitu kama hiko hii sheria imetungwa hasa kuzilinda timu zisizokuwa na nguvu kiuchumi.

As long mkataba mmeingia watu wawili hata wakati wakuvunjwa lazima pande zote ziliziane.
Barca wakati wanaweka ile release clause ya Neymar walijua ni pesa nyingi ambayo hakuna timu ingeweza kuufikia

Kama ni kweli Yanga waliweka kipengele hicho kwa Fei kwa pesa ile, watakua nao walijua Fei anaipenda Yanga hawezi nunua mkataba wake tena dirisha dogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…