Kuna ubaya wowote kulala hotelini au lodge badala ya kulala msibani pasipo na malazi ya kutosha?

Kuna ubaya wowote kulala hotelini au lodge badala ya kulala msibani pasipo na malazi ya kutosha?

Nyaka-One

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2013
Posts
4,730
Reaction score
6,736
Maisha yetu ya kitanzania wote tunayafahamu. Nimemsindikiza rafiki yangu kwenye msiba wa ndugu yake wa karibu na mazishi ni kesho kutwa.

Nikiangalia kwa haraka haraka kwa udogo wa nyumba msiba ulipo na idadi ya waombolezaji ambao wengi wao wanaonekana watalala nataka nimshauri huyu rafiki yangu tutafute mapema vyumba vya kulala kwenye hotel ya kawaida au lodge iliyo jirani ili kuepuka kukosa mahali pa kulala hapa msibani au kubanana kulala kwenye mikeka, ndani ya gari, kwenye masofa, magodoro tupu machache yaliyopo n.k.

Pia kuepuka kushambuliwa na mbu, kuibiwa begi au kuchomolewa vitu kwenye begi n.k. maana kwenye misiba hayo mambo utokea sana.

Ni nini maoni yako wewe mwanaJF kama kuna ubaya wowote wa kutafuta chumba nje ya nyumba msiba ulipo au ni lazima kulala msibani?
 
Hapana ubaya! wewe nenda kalale lodge kama mazingira ya msiba yanaruhusu kupata malazi salama, ingekua ni kijijin huko hata lodge au hotel hakuna hapo ndo sawa! Sioni ubaya mkalale tu

Kwanza misibani huko wengine hufanya sehemu ya kuzagamuana hiyo ndo mbaya zaidi, wengine wanalewa tu hovyo hovyo.

Kama wewe unaenda kupumzika kwa amani huku mkitafakari ya marehemu kuna ubaya gani?
 
Msiba ni kushiriki na wafiwa, kama huwezi kushiriki nao kwa kulala ni bora ungeenda siku ya kuzika na kuondoka. Kila mmoja akiwa na huo utaratibu wa kutafuta pa kulala nje ya msiba tutatengeneza jamii ya aina gani?
 
Hakuna ubaya wowote mkuu. Bora wewe kuliko wanaokesha kwa ulevi kwenye msiba.
Ndo hicho nachokisema wengine wanageuza msiba kama ndo sehemu ya kuzagamuana wake za watu, sana sana hili la ulevi. Misiba ya kibongo ni sometime ya ajabu sana.

Kwanza ukienda lodge kulala unaepukana na vitu vingi.

NB; Ingekua ni kijijini kwamba hakuna access ya hivo vitu sawa.
 
Back
Top Bottom