Kuna ubaya wowote kulala hotelini au lodge badala ya kulala msibani pasipo na malazi ya kutosha?

Kuna ubaya wowote kulala hotelini au lodge badala ya kulala msibani pasipo na malazi ya kutosha?

Kwa tamaduni zetu uwepo wa watu ndio msiba wenyewe, assume kila mtu akaondoka akabakia marehem mwenyewe ndani kisha asbh ndio kila mmoja anajitokeza kurudi.

Mkilala msibani inakuwa rahisi kupangiana majukum asbh ili watu wanapokuja wakute vitu vingi viko katika msitari
 
Wewe lala hapo acha hizo jalibu kuwaza kama ingekua upande wako,watu wamekuja kukufariji mda wa usiku wote watokomee kulala gest, ubaki mwenyewe itakuaje hapo.
 
Sasa nini kimekuwahisha msibani kama kulala huwezi? Ungetenga siku yako yenye haina hizo ghasia ukaebda kuwaona na kuondoka basi.
Alitaka rafiki yake amuone anajali na kutoa kampani, kumbe mtu mwenyewe kaenda huku kachana vindevu vyake na kuvipaka super black, kavaa raba nyeupe na kakoti kake hataki vichafuke na pia anataka usiku apate muda wa kuchat na kupigiana simu vibebi vyake wasimuliane upuuz mwiingi ndo apate usingizi alale.
Msiban ni kulala popote, kula chochote, kushiriki kazi yoyote bila kujali inakuchafua au inakuacha msafi.

Unashindwa kuvimilia kitu cha siku moja tu, si ungebakia huku.
 
Maisha yetu ya kitanzania wote tunayafahamu. Nimemsindikiza rafiki yangu kwenye msiba wa ndugu yake wa karibu na mazishi ni kesho kutwa. Nikiangalia kwa haraka haraka kwa udogo wa nyumba msiba ulipo na idadi ya waombolezaji ambao wengi wao wanaonekana watalala nataka nimshauri huyu rafiki yangu tutafute mapema vyumba vya kulala kwenye hotel ya kawaida au lodge iliyo jirani ili kuepuka kukosa mahali pa kulala hapa msibani au kubanana kulala kwenye mikeka, ndani ya gari, kwenye masofa, magodoro tupu machache yaliyopo n.k. pia kuepuka kushambuliwa na mbu, kuibiwa begi au kuchomolewa vitu kwenye begi n.k. maana kwenye misiba hayo mambo utokea sana. Ni nini maoni yako wewe mwanaJF kama kuna ubaya wowote wa kutafuta chumba nje ya nyumba msiba ulipo au ni lazima kulala msibani?
Si urudi tu huko ulikotoka
 
Msiba ni kushiriki na wafiwa, kama huwezi kushiriki nao kwa kulala ni bora ungeenda siku ya kuzika na kuondoka.
Kila mmoja akiwa na huo utaratibu wa kutafuta pa kulala nje ya msiba tutatengeneza jamii ya aina gani?

Kwani si anaenda kulala lodge muda wa watu wote kulala?

Watu wanakusanyika msibani kwa sababu ya kufarijiana tukio ambalo muda wa kulala huwa halifanyiki...
 
Alitaka rafiki yake amuone anajali na kutoa kampani, kumbe mtu mwenyewe kaenda huku kachana vindevu vyake na kuvipaka super black, kavaa raba nyeupe na kakoti kake hataki vichafuke na pia anataka usiku apate muda wa kuchat na kupigiana simu vibebi vyake wasimuliane upuuz mwiingi ndo apate usingizi alale.
Msiban ni kulala popote, kula chochote, kushiriki kazi yoyote bila kujali inakuchafua au inakuacha msafi.

Unashindwa kuvimilia kitu cha siku moja tu, si ungebakia huku.
Unashindwa kuvimilia kitu cha siku moja tu, si ungebakia huku.

Kweli, jambo la siku moja tu ni nafasi ya kuonyesha upendo japo kwa kujikaza sana watu hawajuagi tu.
 
Kawaida tuu ww kajilalie zako..acha ndugu wapate space..mbona ni kawaida tuu siku hizi...tena kuna msiba nilienda walikua wanatafutia watu lodge walale...yani mtu upigwe na baridi au mvua mixa mbu wakati wenzio wako ndani wameuchapa..au hata kama hawajauchapa wapo mahali ambapo panavumilika...
 
Maisha yetu ya kitanzania wote tunayafahamu. Nimemsindikiza rafiki yangu kwenye msiba wa ndugu yake wa karibu na mazishi ni kesho kutwa. Nikiangalia kwa haraka haraka kwa udogo wa nyumba msiba ulipo na idadi ya waombolezaji ambao wengi wao wanaonekana watalala nataka nimshauri huyu rafiki yangu tutafute mapema vyumba vya kulala kwenye hotel ya kawaida au lodge iliyo jirani ili kuepuka kukosa mahali pa kulala hapa msibani au kubanana kulala kwenye mikeka, ndani ya gari, kwenye masofa, magodoro tupu machache yaliyopo n.k. pia kuepuka kushambuliwa na mbu, kuibiwa begi au kuchomolewa vitu kwenye begi n.k. maana kwenye misiba hayo mambo utokea sana. Ni nini maoni yako wewe mwanaJF kama kuna ubaya wowote wa kutafuta chumba nje ya nyumba msiba ulipo au ni lazima kulala msibani?
Ubaya upo umeenda msibani kua sehemu ya faraja kwa rafiki ako au ile familia manake kipindi chote cha kuzika utakua nayo kama ungetaka kulala pasipo na mbu ungekaa tu kwako utoe salamu za pole sasa nini maana ya kusindikiza msibani.
 
Msiba ni kushiriki na wafiwa, kama huwezi kushiriki nao kwa kulala ni bora ungeenda siku ya kuzika na kuondoka.
Kila mmoja akiwa na huo utaratibu wa kutafuta pa kulala nje ya msiba tutatengeneza jamii ya aina gani?
Kabisa hiki ulichokisema kina maana sana. Mwenye masikio na asikie.
 
Maisha yetu ya kitanzania wote tunayafahamu. Nimemsindikiza rafiki yangu kwenye msiba wa ndugu yake wa karibu na mazishi ni kesho kutwa.

Nikiangalia kwa haraka haraka kwa udogo wa nyumba msiba ulipo na idadi ya waombolezaji ambao wengi wao wanaonekana watalala nataka nimshauri huyu rafiki yangu tutafute mapema vyumba vya kulala kwenye hotel ya kawaida au lodge iliyo jirani ili kuepuka kukosa mahali pa kulala hapa msibani au kubanana kulala kwenye mikeka, ndani ya gari, kwenye masofa, magodoro tupu machache yaliyopo n.k.

Pia kuepuka kushambuliwa na mbu, kuibiwa begi au kuchomolewa vitu kwenye begi n.k. maana kwenye misiba hayo mambo utokea sana.

Ni nini maoni yako wewe mwanaJF kama kuna ubaya wowote wa kutafuta chumba nje ya nyumba msiba ulipo au ni lazima kulala msibani?
Msiba usiwe mateso kwa wengine! Siku nikifa nitakodi mahema na magodoro watu wasipate shida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom