Kuna ubaya wowote mtu kumpenda mke wa mtu? Mbona Daudi alimpenda mke wa Uria na akabarikiwa?

Kuna ubaya wowote mtu kumpenda mke wa mtu? Mbona Daudi alimpenda mke wa Uria na akabarikiwa?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wana MMU,
Salaam.

Japo mimi sii member active sana humu MMU, ila ni mfuatiliaji mzuri wa mada za MMU.

Kwenye what's app group fulani kuna mjadala kuhusu jamaa fulani kampenda mke wa mtu.

Watu wanajifanya kushangaa sana iweje mtu ampende mke wa mtu?. Wengine hadi wakafikia kumlaani huyu mpendaji kuwa kitendo cha kumpenda mke wa mtu, atalaaniwa!.

Hii ni thread ya swali hypothetical tuu na naliuliza very objectively, kuna ubaya gani mtu kumpenda mke wa mtu?.

What is Love?.
Kupenda is love, ni kitu kinachotokea naturally for a reason au inaweza kutokea tuu for no reason at all!. Sasa ikitokea tuu naturally, mtu kumpenda mke wa mtu mwingine, jee kuna ubaya gani?. NB. Naomba lets underline, kupenda, love na kutoka na mke wa mtu!, hapa nazungumzia ku penda, just imagine wewe ni mwanamke mke wa watu, halafu umependwa na mwanaume mwingine, jee wewe una kosa kupendwa?, kwani ni wewe ndio umemwambia huyo mwanamume, akupende?.
Jee Wanawake Wanahitaji Nini Ndani ya Ndoa?.
Kitu cha kwanza wanawake wote wanachohitaji ndani ya ndoa ni ile amri kuu kupita zote, upendo. Wanawake wanahitaji kupendwa kwa upendo wa dhati, ila pia wanahiji kutimiziwa mahitaji yao yote, na kulishwa vizuri hadi wakatosheka. Pakiwepo na upendo wa dhati, hata asipotimiziwa mengine yote, hata akilazwa na njaa, upendo utavumilia, yaani love will conquer all.

Jee Wake Wote wa Watu Wanapendwa na Waume Zao?.
Kuna wanawake wengi sana wanaishi kwenye ndoa za mateso, na kiukweli hawana mapenzi kabisa toka kwa waume zao, na kuna wengine wanapendwa lakini waume zao hawana uwezo wa kuwatimizia wakatosheka. Sasa kuna ubaya gani mtu baki, ukampenda mwanamke kama huyu na ukamtimizia akatosheka?

Jee Wake Wote wa Watu Wanatimiziwa na Waume Zao?.
Jibu ni hapana, sii wake wote wa watu wanatimiziwa. Ikumbukwe ndani ya ndoa, mke kutimiziwa mahitaji yake yote sio hisani ya mume, ni wajibu wa mume. Hapa nazungumzia kutimiziwa mahitaji yote, ya kidunia, kimwili na kiroho, na wale wanaotimiziwa, sii lazima mahitaji yote yatimie, Sasa ikitokea mtu akampenda mke wa mtu asiyetimiziwa mahitaji yote na mumewe, na wewe ukajikuta una uwezo wa kumtimizia mahitaji yake yote, jee kuna ubaya wowote kumtimizia hayo mahitaji ambayo mumewe ameshindwa kuyatimiza?.

Jee Wake Wote wa Watu, Wanatoshelezwa na Waume Zao?.
Jibu ni hapana, sio wanawake wote wanatoshelezwa na waume zao na wakatosheka. Ikumbuke kutosheka sio sio suala la kutimiziwa tuu mahitaji, unaweza kutimiziwa mahitaji yote na yakatimia lakini ukajikuta hujatosheka!, kama kilivyo chakula, unaweza kula na ukashiba lakini ukawa hujatosheka, mfano wewe unapenda kula ugali mgumu wa muhogo wa Jangombe, lakini chakula kinachopikwa kwako ni ubwabwa boko boko au wali wa nazi aliopikiwa mtoto, ukishindilia huo ubwabwa tumboni, utashiba, lakini bado utakuwa hujatosheka, ili utosheke, shurti upate muhogo, Sasa ikitokea hawa wake za watu, wanaolazwa njaa kila uchao, kufuatia kutotosheka chakula cha nyumbani kwao, na wewe ukajikuta unampenda na unaweza kumtosheleza kwa kumshibisha, kuna ubaya ukimshibisha?.

True Story ya Ujana Maji ya Moto, Tulitimizia, Tosheleza na Shibisha Hivyo na Wakadumisha Ndoa Zao.
This is a true story ya enzi za ujana maji ya moto, sisi ndio vijana machachari damu inachemka, tumemaliza shule pale TSJ, ikiwa Ilala, tukaajiriwa kazi RTD, tukapangiwa flat ya Da Mwajuma Mchuka pale Ilala Shariff Shamba, watangazaji vijana, enzi hizo Tanzania redio ni moja tuu RTD, you can just imagine!. Ni katika ujana huo, ndipo tukajifunza kumbe kuna wanawake wengi sana ni wake za watu, wanaishi kwenye ndoa za mateso, zisizo na upendo, wanaume walevi hawana uwezo wa kuwatimizia wake zao, na kuna wanawake kibao wanakula lakini hawashibi!, sasa katika mazingira kama hayo, tulikutana na wengi waliokata tamaa kabisa kuendelea na ndoa zao, lakini baada ya kupendwa na watu baki, wakatimiziwa mahitaji yao yote ambayo waume zao wameshindwa kutimiza, na wakashibishwa, hivyo kutoendelea kulala njaa, walitulia kwenye ndoa zao, hivyo ni sisi ndio tuliosaidia kudumisha ndoa zile!, jee hili sii jambo jema?.

Tofauti ya Kupenda na Kutamani!. Kupenda ni Jambo la Kheri na Kutamani ni Dhambi.
Kupenda ni Love, na kutamani ni Lust. Amri kuu kuliko zote ni upendo, hivyo kumpenda mtu yoyote hata akiwa ni mke wa mtu ni jambo la kheri, lakini kutamani mke wa mtu ndio dhambi, Ila ikitokea mtu ukampenda mke wa mtu aliyekosa upendo kwa mumewe, na ukamtimizia mahitaji aliyokosa kwa mumewe, na ukamtosheleza anavyoshindwa kutoshelezwa na mumewe, sio tuu utapata baraka za kumsaidia mwanamke huyo, bali pia utapata baraka za mumewe, kwa sababu unamsaidia kutimiza majukumu ambayo ni ya kwake!.

Mfalme Daudi Japo Alimtamani Mke wa Mtu, Akampata Kwa Dhambi, Na Bado Alibarikiwa!.
Kwa msio mjua Mfalme Daudi, ni yule kijana mdogo aliyempiga Goliati, akawa Mflme wa Israel. Akamtamani mke wa jemedari wake aliyeitwa Uria, hivyo akamtuma huyo jemedari vitani ili auwawe, na kweli Uria alipokufa, akamtwaa mkewe, Bersheba, na kumfanya ni mke wake!. Japo Daudi alifanya dhambi ya kumtamani mke wa mtu, lakini kitendo cha Daudi kumtwaa na kumpenda kwa dhati, kumtimizia mahitaji yake na kumtosheleza, Daudi alibarikiwa, na Bersheba akamzalia mtoto aliyeitwa Sulemani, na ndio aliyeurithi ufalme wa Daudi!. Hizo ni baraka. Sulemani ndio the master lover number moja duniani, haijapata kutokea, alikuwa na wake 700 na masuriya 300, au wake 800, masuriya 200!, ila pia ndie mtu aliyekuwa na busara kuliko binadamu wote, alimpenda Quuen of Sheba, akamuoa, na chini ya ile milima ya Abysinia, ndiko zilikohifadhiwa hazina za Mfalme Suleiman!. Sasa ikitokea kuna mwanamke unampenda, na mumewe hayupo, ukaamua kumsaidia kwa kumtimizia mahitaji yake yote ikiwemo kumshibisha na akashiba, kuna ubaya wowote?.

Somo hili la Daudi na Mke wa Mtu, linatufundisha kuwa njia za Mungu ni tofauti na njia za binaadamu, kuna watu wanafanya dhambi kubwa za ajabu hapa duniani ambao wangestahili hukumu, lakini wanabarikiwa!, na mifano iko mingi jinsi watu wabaya wanavyobarikiwa, huku tukishuhudia jinsi watu wema wanavyoteseka ndani ya dunia hii, mfano hai ni simulizi ya Ayubu, alikuwa mtu mwema lakini angalia kilichompata!. Waovu wanafanikiwa, huku wema wakiamngamia, hivyo nawaombeni sana, kwenye maisha ya dunia hii, tusihukumu, tusije kuhukumiwa!.

Jee Wajua, Hakuna Kosa Lolote La Jinai Mtu Kumpenda Mke wa Mtu na Kumsaidia Mumewe!.
Kuna wengi wamelaumu katika mjadala ule kuwa ni kosa kubwa mtu kumpenda mke wa mtu mwingine, na hata kusema ni dhambi na kuwa atahukumiwa, kiukweli kwa mujibu wa sheria za Tanzania, sio kosa kwa mtu kumpenda mwanamke yoyote wa umri wowote, ila ni kosa kuwa na mahusiano na mwanamke chini ya umri wa miaka 14, au kama ni mwanafunzi, lakini hakuna kosa lolote la jinai, kumpenda mke wa mtu, na hata ukifanya naye jambo lolote, hakuna jinai yoyote, unless kama uli mbaka!, lakini watu wazima na akili zao, kuwa na mahusiano yoyote binafsi, hakuna kosa lolote la jinai!, japo kuna crimes against morality, hazishitakiwa mahakamani!.
Hitimisho.
Wanawake, ni mama zetu, dada zetu na wake zetu, wengi wao wanaishi kwenye ndoa za mateso, hawapendwi, hawatimiziwi, hawatoshelezwi, sasa katika safari ya kuelekea kwenye usawa wa kijinsia, kama sisi wanaume tulivyo na uhuru wa kupenda mtu zaidi ya mmoja na isinekane ni jambo la ajabu, its high time, tuwape uhuru huo wa kupenda na kupendwa, mama zetu, dada zetu, na wake zetu.
Namalizia kwa swali hili la msingi, Japo "The Forbidden Fruits the Sweetest", na "Vifunikavyo Vyaliwa, Vyaachwa Vilo Wazi", Jee ikitokea mtu kumpenda mke wa mtu mwingine, jee kuna ubaya gani?.

Ila pia pamoja na yote, mwisho wa yote ni hukumu ya haki iitwayo karma, ambayo kila binadamu atahukumiwa kwa kadri ya wema wake!, unaweza kumpenda mke wa mtu kwa lengo la kumsaidia yeye na familia yake, ukapata baraka kwa usaidizi huo, na unaweza kumpenda mke wa mtu, kwa dhambi ya matamanio ya mwili tuu, na hivyo kumuangamiza mume wake na kuisambaratisha familia yake, japo kidunia unaweza kufanikiwa sana, lakini mwisho wa siku lazima karma itakuhusu!.

Muongozo wa kuujadili uzi huu:
Nasisitiza uzi huu ni hypothetical situation, hivyo nawaombeni sana, msiingize jina la mtu yoyote, na pia isiiamini sana taarifa za umbeya wa mitandaoni kuhusu wake za watu!.
Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa ...

Nawatakia Jumatano Njema.
Paskali
Rejea
Enyi Waume Wapendeni Wake Zenu!-Wife Kanirudia Saa12:00 Asubuhi ...
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya ... - JamiiForums

 
Wana MMU,
Salaam.

Japo mimi sii member active sana humu MMU, ila ni mfuatiliaji mzuri wa mada za MMU.

Kwenye what's app group fulani kuna mjadala kuhusu jamaa fulani kampenda mke wa mtu.

Watu wanajifanya kushangaa sana iweje mtu ampende mke wa mtu?. Wengine hadi wakafikia kumlaani kuwa atalaaniwa!.

Hapa nauliza very objectively, kuna ubaya gani mtu kumpenda mke wa mtu?.

Jee Wake Wote wa Watu Wanapendwa na Waume Zao?.
Kuna wanawake wengi sana wanaishi kwenye ndoa za mateso, na kiukweli hawana mapenzi kabisa toka kwa waume zao, na kuna wengine wanapendwa lakini waume zao hawana uwezo wa kuwatimizia wakatosheka. Sasa kuna ubaya gani
mtu baki, ukampenda mwanamke
kama huyu na ukamtimizia akatosheka?.
Jee Wake Wote wa Watu Wanatimiziwa?, Wanatoshelezwa?.
Jibu ni hapana, sii wake wote wa watu wanatimiziwa, na wale wanaotimiziwa, sii lazima wanatoshelezwa. Sasa ikitokea mtu akampenda mke wa mtu asiyetimiziwa, ukamtimizia, au asiyetoshelezwa, ukamtosheleza, kuna ubaya gani?.
True Story ya Ujana Maji ya Moto, Tulitimizia, Tukatosheleza na Kuwadumishia Ndoa.
This is a true
Kuna hisia za ndani sana juu ya mwanamke unapongundua anatoa penzi nje hata kama humpendi sana.
Na ni mbaya zaidi kama bado unaishi naye nyumba moja.

Ni bora akafanya hayo akiwa mbali na wewe kidogo.

Mambo ya mahusiano ni magumu kiasi fulani kwani yamejikita ndani kabisa ya hisia za mwanadamu.
 
Wana MMU,
Salaam.

Japo mimi sii member active sana humu MMU, ila ni mfuatiliaji mzuri wa mada za MMU.

Kwenye what's app group fulani kuna mjadala kuhusu jamaa fulani kampenda mke wa mtu.


True Story ya Ujana Maji ya Moto, Tulitimizia, Tukatosheleza na Kuwadumishia Ndoa.
This is a true


Raisi wa nchi huwa anamkulia wapi huyo mama? Kwa maana raisi wetu hatoki nje ya nchi, sasa raisi anawezaje tu kutembea na Waziri kirahisi rahisi hivi hivi? Mmemtafuuta koote raisi wetu mmemshindwa sasa mnaaza character assassination, ...
 
Bebi kaolewa na nani?

Duh, Magu kafika bei pale?

Cha Arusha atakiweza?


Nashangaa leo baby kabae anaponda koti na suti ya maalim seif nahuku siku mbatizaj aiposema anataman waje na familia zao pale 360 niliona aibu mm !koti alilovaa mumewe jaman khaaaaaa ! kuuubwaaaaaaaa na mwanaume mwembamba bas kafunikwa balaaaaaaaaa ova housboy wake !mhhh
 
Back
Top Bottom