Kuna Uchawi au Uganga unaweza kufanya ukaongezwa mshahara au kupandishwa cheo kazini?

Kuna Uchawi au Uganga unaweza kufanya ukaongezwa mshahara au kupandishwa cheo kazini?

I AM NO ONE

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2020
Posts
389
Reaction score
576
Habari,

Aise mimi kuna mahali nafanya kazi ila sasa kuna mtu nafanya nae kazi ananiambia we kaa hivyo hivyo usihangaike. Sasa huyo anaenimbia hivyo ni mtu alikuwa kitengo kingine akahamishwa akapelekwa kingine chenye nafuu kidogo

Halafu sasa ananiambia kashapewa barua ya kuongezewa mshahara ila sasa usemi wake kila akiniona ofisini ananiambia mdogo wangu karoge, hangaika

Je, naomba kujua kama kuna ushuhuda wa ukweli kuhusu uchawi wa namna hii upo kweli?
 
Performance ya mtu pamoja na nidhamu ya kazi ndio inampa mtu nafasi ya kukua kazini. Inaelekea huyo rafiki yako anavyo vyote ila sababu anaamini kwenye hizo mambo basi ataona ndio zinamsaidia kumbe juhudi yake binafsi na mapenzi ya Mungu vinatosha
 
Hana juhudi yoyote tena ni msufumbu hatari mpka hao mabosi walishampa barua ya kumkanya, halafu anagombana sana na wateja
 
Basi maisha yangekua simple sana, watu tusingekubali kupoteza pesa kusomesha watoto wetu wakati kwa mganga mambo supa

Lakini hata hivyo tungeona zile department nyeti zina endeshwa na mabosi waganga ambao wamekubuhu kwa uchawi
 
Back
Top Bottom