Kuna udhaifu mkubwa katika teknolojia inayochukua kumbukumbu za kadi ya mpiga kura

Kuna udhaifu mkubwa katika teknolojia inayochukua kumbukumbu za kadi ya mpiga kura

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2014
Posts
530
Reaction score
1,446
Ningependa kushare na nyinyi kile ambacho nimebaini, ingawa siyo mhusika wala msimamizi/mwandikishaji.

Majuzi, tarehe 5, nilikwenda Katoro kwenye kata yangu na kuamua kubadilisha kadi yangu ya mpiga kura ili kurekebisha taarifa, saini, na picha. Nilipofika kwenye kata moja, nilipanga mstari na kadi yangu ya zamani mkononi. Zamu yangu ilipofika, niliandikisha kwenye fomu mpya, ingawa mimi binafsi nilitaka kuandikisha fomu ya kubadilisha taarifa badala yake nilipewa fomu ya kuandikisha upya na siyo kubadilisha taarifa.

Nikiwa na kadi yangu ya zamani, walinipa fomu mpya na kwamba nijiandikishe upya, huku nikiwa na kadi ya zamani iliyokuwa na namba T-1005-0988----. Kadi hiyo ya zamani ilikuwa bado na taarifa zangu kama kawaida.

Nikushangaze kidogo;

Leo, nikaenda Bukombe, nikasema ngoja nijaribu tena kuandikisha ili kufufua kadi yangu ya zamani na kupima mfumo huu wa kuandikisha wapiga kura. Katika utaratibu huu, niliandikishwa katika fomu ya kubadilisha taarifa hivyo nikapewa kadi yenye namba zile zile kutoka kwenye kadi yangu ya zamani ambayo niliiacha Katoro baada ya kunipa kadi mpya. Kwa sasa, ninakadi mbili za kupigia kura: moja kutoka Katoro na nyingine kutoka Bukombe-Ushirombo.

Hata hivyo katika utaratibu wote kuanzia Katoro hadi Ushirombo niliombwa namba ya NIDA.

Na kote nimeweka namba ya NIDA pamoja na kuwapa bado hawajanitambua kuwa nimeandikiswa sehemu nyingine.

Hii inaonyesha kwamba mfumo wa kuandikisha kadi za kura hauna ulinzi wa data wa kutosha, au pengine hili siyo kipaumbele kwa TUME HURU YA UCHAGUZI, huenda kipaumbele cha Tume ni kutimiza takwa la kila mwananchi aliyetimiza umri wa kupiga kura anapata kadi bila kuzingatia kama tayari ana kadi au laah. Hii inazidi kunipa mashaka kuhusu usalama wa mifumo yetu ya kupigia kura.

Kama TUME HURU YA UCHAGUZI imo humu wajitafakari au kama wataipata post hii basi wajue wapi wanatakiwa kufanya marekebisho ya haraka zaidi huenda hili walikuwa hawalijui au wanalijua ila wamekaza tu kwamba hakuna anaejua hili
 
Hili nalo likafanyiwe kazi km inaitajika kurekebishwa au km ndivyo inatakiwa kuwa bac watolee maelezo yanayoelewekaa .
 
Ungegundulika ungeingia kwenye matatizo bure,kulikuwa kuna haja gani kujiandikisha mara mbili!
Alikuwa ana testi mitambo, asingejiandikisha mara mbili tusingejua kuwa mtu mmoja anaweza kupiga kura mia mbili kama amejiandikisha mara mia mbili.
 
Alikuwa ana testi mitambo, asingejiandikisha mara mbili tusingejua kuwa mtu mmoja anaweza kupiga kura mia mbili kama amejiandikisha mara mia mbili.
Na kilichonifanya nijue mitambo haifanyi kazi sawa sawa nilitumia nakala yangu ile ya zamani ambayo nilikuwa nayo kwenye simu nikasema ngoja niangalie hii kadi inasoma taarifa za wapi nikakuta inasoma zile za miaka ya nyuma ikabidi niende kwenye kituo kingine kuhakiki kama itakuwa imefungwa au itagundulika nimeandikisha mara mbili chakushangaza hakuna aliyejua wala hamna aliyeniambia chochote nimepewa kadi yangu nakusepa
 
Kujiandikisha mara mbili ni kosa kisheria ,hapo katoro mwendesha VIFAA VYA ELEKTRONIK hakuwa na ELIMU sahihi ya VIFAA .Pale Kuna kifaa kinaitwa KIFAA kina DATABASE ya nchi nzima ilitakiwa akusearch tu angekuona .Ila kwa ushauri tu usimiliki kadi mbili
 
Back
Top Bottom