Kuna Uhalali au ulazima kwa kampuni za simu kutoa namba za simu za mtumba (zilizotumika na watu wengine walio hai au kufa)?

Ni makosa makubwa.
Namba ya simu ingechukuliwa kama ilivyo Namba ya nida siyo inabadilishwa kama chupi ya mtumba mwaka huu kavaa mchina miezi sita baadaye anayo mzaramo wa msanga ngongele.
 
Mi yangu niliipoteza nikataka kuirudisha nashangaa!Kapewa mchina!
 
Shida tupo vizuri sana kwenye mikakati njoo utekelezaji ni aibu.
Uko wapi mfumo wa tiketi mtandao?
Ukiingia unakuta kampuni kadhaa zimeweka mabasi yao wengine hawaweki.
Mtu ukitaka kusafiri mpaka uanze kutafuta tiketi kwenye mfumo wa basi binafsi. Wakati lile wazo lilikuwa zuri, serikali ingefanya monitoring ikalipwa kusimamia mfumo na kampuni zote zikafanya kazi kisheria bila kuibia abiria.
Na bado kampuni zingine hazitumii mfumo wa electronics kabisa iwe tiketi ama mfumo hawana. Ukiwauliza majibu mepesi kabisa na wasimamizi wapo.
Inahuzunisha sana.
 
Kwanini wasiziondoe tu kwenye
system?
 
Mimi kuna number nilipoteza aisee watakae mpa na mhurumia, ina deni la nipige tafu 10k.. Songesha 70k so atajuta.
 
Hawaruhusiwi
 
Nasema'ivii, hiyo calculation ni ya uongo.

Je nchi zenye raia wengi kama mchwa wanaozidi billion, wanadhibitiwa kumiliki #za simu?

Halafu namba anayonyang'anywa mtu kwanini iwe tamu sana kuuzika sokoni wakati kuna mrundikano wa line mpya kwa vendor hazina hata wa kuzinunua?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…