howardlite
JF-Expert Member
- Jul 16, 2016
- 242
- 392
Ndugu Watanzania wenzangu nawasalimu,
Zipo nadharia nyingi kuhusu Ugojwa wa Corona, na kumekuwa na jitihada nyingi za ndani na nje ya nchi yetu za kupambana na virusi hivi vinavyotishia ustawi wa sayari yetu.
Tumekuwa tukisikia tahadhari nyingi kuhusu matumizi ya Chanjo (Vaccines) za Corona, lakini hakuna majibu yanayoondoa mashaka ya tahadhari hizo.
Nani wakuondoa maswali haya tata kuhusu kinachoelezwa juu ya kinachoitwa madhara ya chanjo za Corona? Je, ni serekali? Viongozi wa dini? Wanasiasa? Madaktari? Shirika la Afya (WHO)? Au ni nani?
Nani wa kuaminiwa, nani wa kuondoa mashaka haya?
Maendeleo yoyote katika nyanja yoyote ya maisha yanategemea "watu", Watanzania kwanza maendeleo yanafuata.
Viongozi wetu mliopewa nafasi ya kuiongoza nchi yetu na Watanzania wenzenu, mna dhamana ya uhai wa maisha ya Watanzania na vizazi vijavyo.
Kama kuna mambo mnayajua nyuma ya pazia kuhusu Corona na chanjo zake ambayo yanaweza kuligharimu hili taifa na vizazi kwa vizazi, Mwenyezi Mungu yupo muogopeni yeye, ponyeni nafsi zisizo na hatia. Simameni kwenye kweli ya maisha ya Watanzania wenzenu hata kama kuna gharama, hakuna mbadala wa uhai wa watu.
Jaribuni kuona matamko mnayoyatoa kuhusu Corona na muitikio wa watu wenu, je haitufundishi kitu? Watu hawaelewi? Sio kweli. Kuna mahali labda hatujakuwa wazi kwa sababu tunazozijua Kama Viongozi? Tunaogopa kuusema ukweli? Kuna ulaghai? Ubinafsi? Au matishio?
Heri wenye dhamiri safi za mioyo yao kama viongozi, maana wataliponya taifa letu, maisha yetu, uchumi wetu na vizazi vyetu na majina yao yataandikwa kwa wino usiofutika.