Kuna uhusiano gani kati ya biashara na paka?

I miss the old days when 'pussy' was another name for cat. Tangu walimwengu muingilie kati kila kitu kimekua tafrani. Hata kua na paka dukani imekua tatizo!
 
Hao ndo chuma ulete mkuu. hao kwa macho ya nyama utaona ni paka ila kiuhalisia(imani) si paka bali ni wafanya kazi wa duka husika.
Kama huamini nenda Singida mjini kaone kwenye maduka.
Biashara zina mambo mengi sana ili ziweze kusonga mbele na waliosomea biashara darasani kwa bahati mbaya sana hawafundishwi kwenye topic zao kuhusu uhalisia.
 
Wachawi utumia paka kama chuma ulete kuchukua pesa dukani ,paka anatumwa kimazingara wewe kama haupo vizuri huwezi muona lakini huyo paka anakuwa ni paka mtu,muuza duka unaweza mtumia paka wa ukweli kumzibiti paka wa kichawi na kuzuia kuibiwa hela kimiujiza watu wa Tanga tunaita kukoperwa.

Hizi habari nilishuhudia kule TANGA maeneo ya Kwa Mkono miaka ya nyuma sana.

Pia Paka ukamata panya ambao ni waaribifu wa bidhaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…