Habari zenu wakuu!
Niende kwenye mada naomba kujua uhusiano uliopo Kati ya mkojo na mimba nikiwa namaanisha kwamba, mwanamke anapohisi ana mimba basi akienda kupima ili kuthibitisha hisia zake, Daktari humpima mkojo na kubaini kama ana mimba au la.
Sasa naomba kufahamishwa kuna uhusiano gani kati ya mkojo na mimba ilihali njia ya mkojo ni tofauti na ile ya uzazi.
Natanguliza shukrani.