Masikini na utulivu wa akili au ustaarabu wapi na wapi ?1. Kwanini kwenye usafiri wa ndege huwa hawapigi mziki mkubwa kama alivyo kwenye basi?, halafu angalia aina ya watu wanaopanda basi na wale wanaopanda ndege.
2. Kwa nini maeneo kama Masaki, upanga na Osterbay hayana kelele , ukilinganisha na Bugurini, Mwananyamala n.k, halafu angalia aina ya watu wanoishi katika naeneo hayo.
3. Kwa nini sehemu za starehe za watu ambao ni high profile huwa hazina mziki mkubwa ukilinganisha na zile za makabwela?
Kwa nini vyumba za kupanga huwa zina kelele ya mziki mkubwa, tofauti na nyumba ambazo wanaishi wamiliki wa hizo nyumba.
Swala hili limenisumbua sana naomba maoni na mtazamo wenu.