Kuna ukweli gani kuhusu watoto wanaofuatana kuzaliwa kupenda kugombana?

Kuna ukweli gani kuhusu watoto wanaofuatana kuzaliwa kupenda kugombana?

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Daaaah nakumbuka wakati nipo mdogo nilikuwa nazichapa haswa na mdogo wangu, ila nilokuwa ni kama napigana kwa tahadhari situmii nguvu zote.

Yaani dogo aliniona mie kama boya tu, saa ikafika siku nikaamua kutumia full force yani nilimshushia mzigo wenyewe bila kujivunga ndio heshima ikawepo.

Hafu ugomvi ukahamia kwake na aliyemfuata, yaani walikuwa wanazichapa haswa.
 
hamna jipya nnachojua mkifatana hamuheshimiani hasa mkizidiana miaka miwili au mitatu unamchukulia kama mwenzio tu.

ila mkipishana miaka 6 kwenda juu huko hapo unamwita kabisa Dada/Kaka na unaamkia.

anyway: mm nnaefatana nae tunaivana tu nna beef ya wakubwa
 
ilo jambo ni kwel mim na dadaangu uwa tunagombana sana, ila nowdays tumekuwa tunaoneana aibu.
 
Hii nimeishuhudia kwetu, mimi na wadogo tumeachana kama mwaka na miezi tu, sasa anayenifuata nakumbuka alikua ananiheshimu japo sinakumbukumbu zakumshushia kichapo.

Balaa lilikua kati yake dogo tumuite Y na dogoo wakumfuata tumuite Z, hapo unakuta Y analetewa dharau au wanagombana na Z lkn kila wakipigana Y anampiga Z, na tatizo nikuwa Z anakibri & jeuri.
Asee ile vita ilikua kubwa mno unaweza ukakaa unashanga mtu anakupita spidi shwaa, ghafla mvua ya mawe inaanza, hapo jua Y katembeza kichapo Z, baada ya hapo Z anajibu mapigo. Hivyo naingilia kati yanaisha.

Kunasiku huyo Z alimzingua Y, na Y akampiga kidogo nakumuacha, ghafla Z akaamka amevimba anataka afuate mawe, nilishuhudia kipigo cha ajabu na nadhani ndiyo ulikua mwisho wa kupigana.

Yule Y alifunguka akampiga bonge la teke la kifua, Z akawa kama amepigwa na upepo wa kisulisuli akazama kwenye uvungu wa meza mixer kumwaga mboga na akakata na moto kwa dakika kadhaa.

Nikashindwa jizuia nikaanza kumshushia kuchapo kwa Y, ghafla Z akazinduka ikabidi tumuangalie hakusema kitu, na toka siku hiyo alitia adabu, hakuwahi kupandisha sauti wala kuleta dharau.

NB: hii vita inaendelea wakati wazazi na wakubwa hawapo, mwisho wa siku wakirudi kila mtu yupo kimya hakuna anaeongea.
 
Mimi na kaka yangu niliemfata na mimi na mdogo wangu wa kiume aliyenifata ile vita ndio ilinifundisha kutumia panga maana ilikua napigwa mande.
 
Sasa hivi naishuhudia vita nyingine kwa watoto wangu wa mwisho waliofuatana ni wa kike hata nikiwepo nyumbani usiku hawalali bila hazijadundwa kwanza.
 
Mimi kaka angu aliyenitangulia alikua ananidunda balaa yani adi nilikua simpendi nikifanya kosa yeye ndo kimbelembele kunipiga mama anamwambia piga reception iache
 
tatizo linakuwa zito hasa mkipishana si chini ya miaka mitatu, msione nyumba zipo kimya, watu wanazichapa aisee
 
Mm pamoja na kuzaliwa 13 kwenye familia yetu ila ni yeye tu ndugu yangu ninae mfatia kuzaliwa ndio hata namba yake kwenye simu yangu haipo nawala Sina shida nayo
 
Kuna ka ukweli kidogo kwenye hili,nna vijana wangu wawili hapa mkono unapigwa daily
 
Back
Top Bottom