Hii nimeishuhudia kwetu, mimi na wadogo tumeachana kama mwaka na miezi tu, sasa anayenifuata nakumbuka alikua ananiheshimu japo sinakumbukumbu zakumshushia kichapo.
Balaa lilikua kati yake dogo tumuite Y na dogoo wakumfuata tumuite Z, hapo unakuta Y analetewa dharau au wanagombana na Z lkn kila wakipigana Y anampiga Z, na tatizo nikuwa Z anakibri & jeuri.
Asee ile vita ilikua kubwa mno unaweza ukakaa unashanga mtu anakupita spidi shwaa, ghafla mvua ya mawe inaanza, hapo jua Y katembeza kichapo Z, baada ya hapo Z anajibu mapigo. Hivyo naingilia kati yanaisha.
Kunasiku huyo Z alimzingua Y, na Y akampiga kidogo nakumuacha, ghafla Z akaamka amevimba anataka afuate mawe, nilishuhudia kipigo cha ajabu na nadhani ndiyo ulikua mwisho wa kupigana.
Yule Y alifunguka akampiga bonge la teke la kifua, Z akawa kama amepigwa na upepo wa kisulisuli akazama kwenye uvungu wa meza mixer kumwaga mboga na akakata na moto kwa dakika kadhaa.
Nikashindwa jizuia nikaanza kumshushia kuchapo kwa Y, ghafla Z akazinduka ikabidi tumuangalie hakusema kitu, na toka siku hiyo alitia adabu, hakuwahi kupandisha sauti wala kuleta dharau.
NB: hii vita inaendelea wakati wazazi na wakubwa hawapo, mwisho wa siku wakirudi kila mtu yupo kimya hakuna anaeongea.