sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Huu utapeli hakufanyika kwa Tamaa kama ilivyozoeleka na ndipo napopata mashaka.
Ni ndugu yangu wa karibu naemwamini sana, nilimtumia pesa laki 6 anunue laptop kwajili ya chuoni. sasa nikawa nafatilia hio laptop naona ananipiga sana chenga, nikafikisha hii kero kwa mama yake ambae ni mamdogo wangu ndio akaelezea kilichomkuta ambacho hadi sasa nahisi ni stori ya uwongo.
Kwamba aliulizwa njia ya kwenda sehem flani, yeye badala ya kuelekeza njia akaanza kumpeleka mtu asiemjua hio sehemu wakati aliulizwa tu njia, njiani wakakutana na mtu mwengine alietoa msaada kumsindikiza huyo alieomba maelezo ya njia.
kufika huko, yule wanaemsindikiza alishukuru sana akawaambia yeye ni mtoto wa chifu na ni mtaalam hivyo atawatolea matatizo yao bure ikiwa kama asante, akaanza na huyu ndugu yangu akamwambia amerogwa, wachawi wameficha nywele kwenye tumbo lake, ndugu yangu akaanza kutema nywele mdomoni, Narudia tena "kutema nywele!"
akaambiwa aende kutoa pesa kibandani, akazitoa zote bila kujielewa, hakuambiwa kwamba hela zitaongezeka au atakuwa tajiri kama ilivyozoeleka, alimwambiwa tu akazitoe, akajikuta anaenda kibandani kutoa zote.
pesa aliondoka nazo akiwa kahakikisha zipo mfukoni, ila anafika kwake anakuta simu imekuwa mbao na hela zote zimekuwa makaratasi ya maboksi.
..............................
Binafsi nimeumia sana, hio pesa inaweza kuwa si chochote kwa mwengine ila kwangu hio laki 6 ni sehem kubwa katika mshahara wangu, Nmeumia mno.
Sasa nmekuja humu kwenye jukwaa la wananchi mnipe ukweli wowote juu ya hii stori maana imekaa kama imetungwa hivi
Pia soma
- Ni namna gani ya kukabiliana na wizi wa kusemeshwa na mtu usiyemjua?