Kuna ukweli wowote katika aina hii ya utapeli?

Kuna ukweli wowote katika aina hii ya utapeli?

Mnunulie Laptop Nyingine Usifukue makaburi Unapoteza Muda! Kama huna hela mwambie sina...
 
Kuna kitu inaitwa Hypnosis. Unakuwa unakubali tu suggestion. Upo kama haupo. Haina uchawi wowote.
 
Jitahidi ufanye mambo yako mwenyewe utalaumu watu bure pesa haina rafiki na haipatikani kizembe
Huu utapeli hakufanyika kwa Tamaa kama ilivyozoeleka na ndipo napopata mashaka.


Ni ndugu yangu wa karibu naemwamini sana, nilimtumia pesa laki 6 anunue laptop kwajili ya chuoni. sasa nikawa nafatilia hio laptop naona ananipiga sana chenga, nikafikisha hii kero kwa mama yake ambae ni mamdogo wangu ndio akaelezea kilichomkuta ambacho hadi sasa nahisi ni stori ya uwongo.

Kwamba aliulizwa njia ya kwenda sehem flani, yeye badala ya kuelekeza njia akaanza kumpeleka mtu asiemjua hio sehemu wakati aliulizwa tu njia, njiani wakakutana na mtu mwengine alietoa msaada kumsindikiza huyo alieomba maelezo ya njia.

kufika huko, yule wanaemsindikiza alishukuru sana akawaambia yeye ni mtoto wa chifu na ni mtaalam hivyo atawatolea matatizo yao bure ikiwa kama asante, akaanza na huyu ndugu yangu akamwambia amerogwa, wachawi wameficha nywele kwenye tumbo lake, ndugu yangu akaanza kutema nywele mdomoni, Narudia tena "kutema nywele!"

akaambiwa aende kutoa pesa kibandani, akazitoa zote bila kujielewa, hakuambiwa kwamba hela zitaongezeka au atakuwa tajiri kama ilivyozoeleka, alimwambiwa tu akazitoe, akajikuta anaenda kibandani kutoa zote.

pesa aliondoka nazo akiwa kahakikisha zipo mfukoni, ila anafika kwake anakuta simu imekuwa mbao na hela zote zimekuwa makaratasi ya maboksi.

..............................

Binafsi nimeumia sana, hio pesa inaweza kuwa si chochote kwa mwengine ila kwangu hio laki 6 ni sehem kubwa katika mshahara wangu, Nmeumia mno.

Sasa nmekuja humu kwenye jukwaa la wananchi mnipe ukweli wowote juu ya hii stori maana imekaa kama imetungwa hivi
 
Kakutana na wale wataalamu. Kwakweli hayajawahi kunikuta ila sijawahi elewa how do they do it
Kuna mtu wangu nilimpa mtaji wa 2.5ml aanze m pesa ndani ya siku 2 akalizwa hivhivi
 
Inawezekana kweli wajanja wamemtaimu,hasa kama ni mgeni wa mji na kila kitu anashangaa shangaa tu...... matapeli Wana Psychologia kubwa kuliko hata Prof of Psychology ya chuo kikuu
Yes hivi karibu kuna msichana alipigwa hivi hivi tena pesa alitoa mwenyewe akamkabidhi akakosa hadi nauli
 
Kuna mtu wangu nilimpa mtaji wa 2.5ml aanze m pesa ndani ya siku 2 akalizwa hivhivi
Dah hasara juu ya hasara. Kuna dogo ye aliwekwa awe wakala akapgwa mls 7 eti anaambiwa atapelekwa marekan
 
Ipo mwenyewe nilibeba mpaka simu ya mama nikawapelekea
 
Iliwahi nikuta hiyo lakini waliishia kwa afande sabasita kituo kikuu cha polisi Morogoro miaka ile.
 
Huo utapel upo mkuu. Wakati hao wahuni wanaku attack anajua 1, anakusimamisha anakuomba msaada wa kuelekezwa njia, hapo hapo anakuja mhuni mwingine anapita kisha na yeye anasaidia kuelekeza, mara utasikia tumsindikize, ukienda kuna chochoro yule wa pili ataelekeza shortcut, mkipita mkishafika kwenye target yao kwa Arusha ni wanakukaba wanachukua hasina zao wanaondoka.
 
Walinikosakosa mtaa Kipata miaka ya nyuma.
Ukipigwa ni ujinga tu, mjanja hapigwi mazee.
 
Umenikumbusha studio pale kinondoni mkaka yule huruma yangu ikaniponza kumbe ndo naenda kupigwa simu na pesa
 
We unaweza cheza na akili ya mtu mpaka aende atm atoe pesa yote akupe pasipo yeye kuwa na ufahamu?
Si kawaida
Ni kwasababu Tu umeshaisikia...ila kama hujui hata wewe wanaweza kukupiga kama unaamini mambo ya uchawi ndio unakuwa vulnerable kabisa...wanajua kucheza Na saikolojia
 
Ni kwasababu Tu umeshaisikia...ila kama hujui hata wewe wanaweza kukupiga kama unaamini mambo ya uchawi ndio unakuwa vulnerable kabisa...wanajua kucheza Na saikolojia
Kwakweli tamaa ndo msingi wa kutapeliwa
 
Back
Top Bottom