macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 25,191
- 48,765
Wanatoa kwa sababu ya ujuha na ushamba wao tu na siyo kwa sababu ya dawa. Tena wastaafu ndiyo wanapigwa kweli kweli.Hii ipo kabisa, una mzee mmoja mstaafu wa mtaani kwetu alipigwa, tena yeye alienda atm mbili tofauti kutoa mpunga.
Kumjua mtua aliyetapeliwa hakumaanishi walitumia dawa. Wanapigwa kwa ujuha na tamaa zao za fedha tuHii ipo asee, kuna dogo langu alipigwa kwa namna hii.
Nasubiri kipenziNgoja nije
Huenda kuna kweli hapa. Binafsi sijawahi kuibiwa kwa namna hii.Wanapigwa kwa ujuha na tamaa zao za fedha tu
Inaonekana walikunyosha vilivyoSitasahau [emoji1430][emoji1430][emoji1430][emoji1430]Pale mwenge mimi🥲🥲
Huu utapeli hakufanyika kwa Tamaa kama ilivyozoeleka na ndipo napopata mashaka.
Ni ndugu yangu wa karibu naemwamini sana, nilimtumia pesa laki 6 anunue laptop kwajili ya chuoni. sasa nikawa nafatilia hio laptop naona ananipiga sana chenga, nikafikisha hii kero kwa mama yake ambae ni mamdogo wangu ndio akaelezea kilichomkuta ambacho hadi sasa nahisi ni stori ya uwongo.
Kwamba aliulizwa njia ya kwenda sehem flani, yeye badala ya kuelekeza njia akaanza kumpeleka mtu asiemjua hio sehemu wakati aliulizwa tu njia, njiani wakakutana na mtu mwengine alietoa msaada kumsindikiza huyo alieomba maelezo ya njia.
kufika huko, yule wanaemsindikiza alishukuru sana akawaambia yeye ni mtoto wa chifu na ni mtaalam hivyo atawatolea matatizo yao bure ikiwa kama asante, akaanza na huyu ndugu yangu akamwambia amerogwa, wachawi wameficha nywele kwenye tumbo lake, ndugu yangu akaanza kutema nywele mdomoni, Narudia tena "kutema nywele!"
akaambiwa aende kutoa pesa kibandani, akazitoa zote bila kujielewa, hakuambiwa kwamba hela zitaongezeka au atakuwa tajiri kama ilivyozoeleka, alimwambiwa tu akazitoe, akajikuta anaenda kibandani kutoa zote.
pesa aliondoka nazo akiwa kahakikisha zipo mfukoni, ila anafika kwake anakuta simu imekuwa mbao na hela zote zimekuwa makaratasi ya maboksi.
..............................
Binafsi nimeumia sana, hio pesa inaweza kuwa si chochote kwa mwengine ila kwangu hio laki 6 ni sehem kubwa katika mshahara wangu, Nmeumia mno.
Sasa nmekuja humu kwenye jukwaa la wananchi mnipe ukweli wowote juu ya hii stori maana imekaa kama imetungwa hivi
Kuna mtu wangu nilimpa mtaji wa 2.5ml aanze m pesa ndani ya siku 2 akalizwa hivhiviKakutana na wale wataalamu. Kwakweli hayajawahi kunikuta ila sijawahi elewa how do they do it
Yes hivi karibu kuna msichana alipigwa hivi hivi tena pesa alitoa mwenyewe akamkabidhi akakosa hadi nauliInawezekana kweli wajanja wamemtaimu,hasa kama ni mgeni wa mji na kila kitu anashangaa shangaa tu...... matapeli Wana Psychologia kubwa kuliko hata Prof of Psychology ya chuo kikuu
Dah hasara juu ya hasara. Kuna dogo ye aliwekwa awe wakala akapgwa mls 7 eti anaambiwa atapelekwa marekanKuna mtu wangu nilimpa mtaji wa 2.5ml aanze m pesa ndani ya siku 2 akalizwa hivhivi
Ni kwasababu Tu umeshaisikia...ila kama hujui hata wewe wanaweza kukupiga kama unaamini mambo ya uchawi ndio unakuwa vulnerable kabisa...wanajua kucheza Na saikolojiaWe unaweza cheza na akili ya mtu mpaka aende atm atoe pesa yote akupe pasipo yeye kuwa na ufahamu?
Si kawaida
Kwakweli tamaa ndo msingi wa kutapeliwaNi kwasababu Tu umeshaisikia...ila kama hujui hata wewe wanaweza kukupiga kama unaamini mambo ya uchawi ndio unakuwa vulnerable kabisa...wanajua kucheza Na saikolojia
Katika hili tukio tamaa haijahusikaKwakweli tamaa ndo msingi wa kutapeliwa