Kuna ukweli wowote kuhusu biashara ya mtandao?

Kuna ukweli wowote kuhusu biashara ya mtandao?

Juma WALEO

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2014
Posts
204
Reaction score
40
Weng wamekuwa wakizungumza kuwa unaweza kufanikiwa kupitia biashara hiyo nahitaji maelezo ya kina kujua inafanyikaje?
 
Mkuu mie kwa uelewa wangu finyu naona hiyo biashara ni kama biashara kichaa vile.
Hii biashar ni kuwa unakuwa unatengeneza chain ya watu ambao watakuwa wanaingia kwa jina lako so wao wanasema kuwa unakuwa unapata nyota kwa kadiri unavyopata watu wengi. Hapo ishu inakuja kwenye kuwashawushi hao watu. Hapo ni lazima uwe kama mmachinga anaeuza bidhaa za promotion.
Maana mpo kwenye semina unaanza kumwaga somo "ooh hii sabuni inatoa mapunye na blah blah kibao. Mara ooh hii dawa ya meno ni nzuri na haina floride na salama zaidi maana ni alovera....blah blah blah...."
Na hapo huna hakika sana kama na soko pia litakuwepo au lah! Nilikuwa na jamaa yangu alikuwa forever living yaani alikuwa ni kama chizi na mbaya zaidi biashara ilikuwa inamkata kila inayoitwa leo. Hana hata hamu.
In short kama wewe ni great orator you may go for it ila sio inalipa kama wao wanavyosema na hizo nyota zao.
All the best
 
Nimekusoma prince!
nimependa maelezo yako
 
Naitamani ila hapo kwenye kuconvince watu ndo patanishinda.maana sina uvumilivu kabisaaa
 
Muanzisha mada hii, nakuomba uende kusikiliza mafunzo yao wanayotoa, jitahidi sana kuwa mtembezi wa mikutano yao, msikivu, ninakushauri sana wewe na maamuzi yako ndio viwe jawabu na si kuwahoji wadau ambao hawana majibu ya uhakika zaidi ya kukuangusha kimawazo.
Biashara ya mtandao ni biashara rahisi sana lakini kutokana na watu kuwa na ubinafsi wanahisi ni ngumu tena ya kimachinga
Hebu wasiliana nami 0765903379
 
Unemployment ni zao la kukosa
basic skills za production,taifa
linapuuza kukomaza vyuo vyenye
tija kama Sido na Veta matokeo
yake ni kuwa na Graduates
wasiokuwa na dira mitaani,hawa
ndio wanageuka wahanga wa
hizi kampuni za kiujanjaujanja za
network marketing,ukiuliza
endapo kila mtu akifanya hyo
network marketing nani
atamuuzia nan jibu hamna,haya
haohao wanaojiita watu wa
netwok marketing badala ya
kuumiza vichwa na kuja na
production yao wenyewe ya hzo
food suppliments ili kuua ndege
wawil kwa jiwe moja yani kutoa
ajira na kujiajiri pia, bado
wanategemea imported
products ili wao watembeze
kama MACHINGA na kutoa
maneno mengi ya kuvutia
watu...ndugu zangu inabd
tubadilike sio lazima kuangalia
mafanikio yetu binafsi kwamba
ntaendesha gari na kujenga
nyumba,lazima tufikirie ni namna
gani tulifanye taifa lisonge
mbele,mbona nchi nyingi za asia
wameweza ku-buy class!..Tujikite
kwenye uzalishaji binafsi
otherwise taifa litageuka la
WAMACHINGA...nb:wamachinga ni
wachuuzi wa bidhaa
wasizozitengeneza
wenyewe.........My perspective
kuhusu solution ya
unemployment ni kuwa serikali
ipunguze enrolment ya
graduates badala yake watu
wasomeshwe bure production
na kisha wapatiwe vitendea kazi
baada ya kuhitimu,few years to
come tutaanza kuexport bidhaa
za mbao kama meza na kabati
badala ya ilivyo sasa, unatakiwa
ujisikie aibu ninapokuuzia ugali
wakati mahindi nimenunua
kwako!..
Reply
 
Ni kweli kabisa hatuweza kuendelea, kutengeneza ajira bora( na wala si umachinga) kama hatatuviinua vyuo vya ufunzi na stadi za kazi.Lazima tuweze kuuza vitu nchi kama wengine hata kwa kuiga wanavyofanya na hata kwa kuiba technolojia, na baadaye kuja na technolojia yetu wenyewe.
 
Uelewa wangu wa biashara ya mtandao ulikuwa ni ONLINE MARKETING au INTERNET MARKETING. Hii ni tofauti na huo umachinga wa kutembeza bidhaa au malipo yako kutegemea mnyororo wa watu uliowaingiza kwenye mtandao wako. Mojawapo ya Online/Internet marketing ni kuwa na website ambapo unatangaza bidhaa zako pamoja na kuwa na mfumo wa kuwawezesha wateja kuagiza bidhaa kutoka kwako, kufanya malipo, na hatimaye kuweza kuwafikishia manunuzi yao walipo. Hii biashara ikiishaimarika inalipa ingawa inahitaji mtaji mkubwa kidogo pamoja na gharama kubwa za mwanzo za kujitangaza.
 
Back
Top Bottom