Kuna ukweli wowote wa sadaka kupelekwa Vatican?

Kuna ukweli wowote wa sadaka kupelekwa Vatican?

Habari wana JF kama kichwa hapo juu kinavyojieleza.

Leo kuna rafiki yangu mmoja nimemsikia akisema kuwa kuna sadaka wanazo changia kanisani (Kanisa Katoliki) zinaenda Vatikani. (Yeye ni mkatoliki)

Hili kwangu ndio kwanza nalisikia kwa huyu rafiki yangu, sikutaka kumbishia kwakua mimi sio Mkristo nikajisemea moyoni nitalifanyia kazi nipate uhakika wa hili.

Kama ni kweli inakuaje wao kwa utajili walionao baada ya kutusaidia sisi tuna wasaidia wao?
Katika 2 Wakorintho 9:7, mtume Paulo alisema, “Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. Huku akiwatia moyo waumini wa Korintho watoe kwa ukarimu, Paulo hakutaka watoe zaidi ya uwezo wao, "kwa kusita au kwa kulazimishwa." Muhimu zaidi, alitaka wategemee imani zao za ndani. Kifungu hiki na ibada hii ni ukumbusho kwamba Mungu anajali zaidi nia ya mioyo yetu kuliko matendo yetu.
 
Iko hivi yaani sadaka huwa zinakusanywa kutoka vijijini ndani kabisa huko, makatekista wanazihesabia tena kwa kusimamiwa na watu zaidi ya mmoja, zinaandikwa kiasi halafu katekista anapeleka wilayani

Ikifika wilayani inapelekwa jimboni, yaani mkoani, hapo inapigwa hesabu yote ya mkoa mzima, halafu zinapelekwa makao makuu, hapa naamini wanaingiza bank, zikifika makao makuu sasa ndiyo zinachenjiwa kutoka Tshilingi kwenda Euro zinapelekwa Vatican, sijui kama huo utaratibu wameubadilisha kwa sasa
Ok ahsante mkuu kwa kunijuza
 
maana ya neno KANISA
1.Mwili wa Kristo yaani wafuasi wake Yesu...Biblia inaposema atakuja kulichukua kanisa inamaanisha wakristo waliookoka dunia nzima wanaoishi kwa utakatifu wakimngojea Yesu aje awachukue 1 Thesalonike 4:13-17
2.Maana ya pili ya neno Kanisa ni Jengo la kuabudia kwa wakristo ...kama ambavyo waislamu wana msikiti na wayahudi wana sinagogi + hekalu
3.Maana ya tatu ya neno kanisa ni dhehebu .Dini ya Ukristo kama zilivyo dini zingine zote duniani inayo pia madhehebu .Neno kanisa hutumika kutofautisha dhehebu fulani na fulani kwamfano kanisa la moravian,kanisa katoliki,kanisa la wasabato n.k

Kuhusu matoleo ya SADAKA Biblia inatufundisha kuwa ukishatoa sadaka hupaswi hata kujua hapo kanisani wanaifanyia nini ,Imani yako inapaswa kuwa umemtolea Mungu na sio wanadamu 2 Wakorintho 9:6-7
Hiyo Aya ya mwisho nahisi ndio chanzo Cha kuwepo utitiri wa wachungaji Kila Kona ya nchi maana wameona fursa ya kuwapiga waumini wenye mtizamo kama wako.
 
Sasa kama kila nchi sadaka zinaenda Vatcan, hao jamaa wa Vatcan wanaweza kununua bara la Afrika wakiamua,fikiria kila wiki sadaka zinaenda vatcan, na sio sadaka za Tanzania tu Duniani kote walipo wa Roman catholic,kila wiki sadaka ziende Vatcan miaka yote,
Dini ni biashara
 
Utaratibu wa kanisa KATOLIKI UPO WAZI TEMBELEA Parokia iliyokaribu nawe utapewa taarifa .
 
Kuna katekista mmoja alipokuwa anazipeleka zile hela jimboni,alikuwa anaongozana na mke wake, akifika mjini anaenda kilabuni, piga ugimbi sana, akimaliza hera analudi zake kijijini

Paroko akaja kustukia mchezo, ilibidi asimamishwe, tulikuwa tunamuita anadhambi ya kula sadaka kipindi hicho wakati mdogo, alikuwa na maisha magumu, watoto zake si kuona hata mmoja ingalau kupewa msaada na kanisa, zaidi ya kuishi kwenye dibwi la umaskini, wakati mapadiri na masista walikuwa wanaishi vizuri tu, baada ya kuwa mkubwa nimemsapoti kwa alichokuwa anakifanya, yaani usalishe usipewe hata hela ya sabuni, halafu sadaka wapewe watu wa Vatikani kweli?

Ukatoliki unauonevu mkubwa sana, ni zaidi ya utumwa
Kwa hio walokole wapo sawa kila mmoja kujianzishia kanisa lake na kumiliki kila kitu mwenyewe mfano Gwajiboy.
 
Hiyo Aya ya mwisho nahisi ndio chanzo Cha kuwepo utitiri wa wachungaji Kila Kona ya nchi maana wameona fursa ya kuwapiga waumini wenye mtizamo kama wako.
Sio mtazamo wangu ila ni mtazamo wa kibiblia.Jaribu kufuatilia masomo yanayohusu Sadaka ya Mwalimu Mwakasege utaelewa zaidi.
Blessed is the hand that giveth than the one that taketh Acts 20:35 Proverbs 22:9-19
 
Siyo kweli,Hakuna msikiti unaokusanya hela kupeleka maka,kwanza hatuna utaratibu wa kushea sadaka za msikiti zinatumika msikitini hapohapo hata bakwata ya wilaya hazifiki[emoji2]
Kama kwenu hamna, huko kwingine wanajitoa ndio maana misaada ya kujenga misikiti na kuhudumia inakuja huku, wapo wanaojitoa kwa ajili ya hiyo.
 
Sio mtazamo wangu ila ni mtazamo wa kibiblia.Jaribu kufuatilia masomo yanayohusu Sadaka ya Mwalimu Mwakasege utaelewa zaidi.
Blessed is the hand that giveth than the one that taketh Acts 20:35 Proverbs 22:9-19
Sawa mkono unaotoa ndio unaopokea ila unaangalia na unayempa naona unatafsir vibaya maandiko, alafu Mwakasege ndio nani ? Sie wengine tunamuona wa kawaida tu kama wengine wanaojidai watumishi wa Mungu.
 
Back
Top Bottom