Kuna ulazima gani wa mimi kujenga nyumbani ikiwa mm naishi mjini?

Kuna ulazima gani wa mimi kujenga nyumbani ikiwa mm naishi mjini?

Unalala kwa nani? Ukienda likizo na familia yako unafikia kwa nani?Siku utakuwa na shughuli ya shida au raha kijijini kwenu na watu watakusindikiza huko utadhalilika kuliko maelezo. Jenga hata ndogo tu
 
Inategemeana umetoka familia ya aina gani kiuchumi.

Wengine kwetu hata nyumba za kulala wadogo zetu tuliowaacha kijijini hawana.

Sioni shida kupaboresha ili kuwatengenezea mazingira mazuri.

Tunatofautiana sana kwahiyo angalia mazingira ya kwenu kisha ujiulize kama unaridhika napo au lah.

Nimejenga nyumbani kwasababu najua hali halisi ya nyumbani kwetu.

Nyumba yako ya kuishi jenga popote unapotaka ila ukipata nafasi jenga na boresha mazingira ya nyumbani kwenu kijijini pia.

Zaidi ya yote angalia kipato chako na fanya maamuzi ambayo hayatakuumiza kiuchumi.
 
Siku ukifa utajua
Asife yeye. Kuna ile unafanya kazi Mbeya na unajenga huko huko Mbeya. Bahati mbaya unafiwa na mwanao unazika Mbeya. Unahamishiwa Bukoba, unapata msiba unazika Bukoba. Wewe mwenyewe unafia Dar....yani mtu anakuwa hana anwani kabisa
 
Back
Top Bottom