Inategemeana umetoka familia ya aina gani kiuchumi.
Wengine kwetu hata nyumba za kulala wadogo zetu tuliowaacha kijijini hawana.
Sioni shida kupaboresha ili kuwatengenezea mazingira mazuri.
Tunatofautiana sana kwahiyo angalia mazingira ya kwenu kisha ujiulize kama unaridhika napo au lah.
Nimejenga nyumbani kwasababu najua hali halisi ya nyumbani kwetu.
Nyumba yako ya kuishi jenga popote unapotaka ila ukipata nafasi jenga na boresha mazingira ya nyumbani kwenu kijijini pia.
Zaidi ya yote angalia kipato chako na fanya maamuzi ambayo hayatakuumiza kiuchumi.