Kuna ulazima wowote kidini au kimila kulia unapofiwa?

Kuna ulazima wowote kidini au kimila kulia unapofiwa?

Nje ya mada, jina lako-Sheilah limenikumbusha classmate wangu wa Primary. Sheilah alikuwa mpole mno, mcheshi na mara nyingi alikuwa na huruma. Kwa udogo wangu ule kipindi hicho darasa la tatu nilikuwa nikimtengenezea picha kichwani akiwa kama mke wangu.

Fast forward tulipofika kidato cha nne alifariki, shida ilikuwa ni ugonjwa wa moyo. Baada ya kufuatilia nilikuja kugundua kwamba hata shule aliyofaulia kidato cha kwanza aliahama kwakuwa ilikuwa kwenye maeneo ya miloma na angeshindwa kupanda na kushuka kila siku.

Tulipokuwa tukisoma nae shule ya msingi kwenye kola ya shati yake aliwekewa kakitambaa kekundu kuonesha alikuwa mgonjwa.

Bahati mbaya hata kufa kwake nilikuja kusikia baada ya miezi kama miwili kupita, nilipatwa na huzuni sana. Ndio maana nilivyoliona jina lako nimekumbuka mbali sana.
 
Siku ukifiwa utajua majibu ya hili ni nini.

Utashika simu ukilia
Utapokea simu ukimaliza kuzungumza utalia
Utakula hata kama ni pilau utakapomaliza tu utalia
Yani utakojoa huku ukilia
Utajipamba lipstick na urembo na bado utalia tu

Kuhandle msiba vizuri?.
Subiri siku yakukute ndio utajua
mtoa mada umewahi kufiwa? na baba, mama, mume, mtoto kaka yako mliyepatana sana umewahi? usijefikiri wanaofiwa wanajifanyisha
Kama kawaida yenu baadhi kwenda kwa mkumbo bila kuelewa context.

Mleta mada anahoji perception ya walioenda msibani kulazimisha wafiwa kulia, mleta mada haoji wafiwa kutolia.
 
Kama kawaida yenu baadhi kwenda kwa mkumbo bila kuelewa context.

Mleta mada anahoji perception ya walioenda msibani kulazimisha wafiwa kulia, mleta mada haoji wafiwa kutolia.
kwani huwa wanalazimishwa kulia??
 
Kama kawaida yenu baadhi kwenda kwa mkumbo bila kuelewa context.

Mleta mada anahoji perception ya walioenda msibani kulazimisha wafiwa kulia, mleta mada haoji wafiwa kutolia.
wewe uliona msiba gani wageni wanafika wanaanza kuwalazimisha wafiwa walie???
 
Watu hawataki kuelewa kwamba kila mtu ana namna yake ya kupitia majonzi.

Na hata kama hajaumia kwa kufiwa na anayesemekana ni mpendwa wake(mtu binafsi ndo anajua nani ni mpendwa kwake), haikuhusu....

Nakumbuka nilipofiwa na mzee sikulia, machungu yalikuja kunishika miezi mingi baadae
Mimi babu yangu alikufa nikiwa likizoni kwake na nikiwa nimemshika, wenzangu wa pembeni wote wanawake. Sikulia wakalia wao tu mimi nikapanga vitu vya muhimu na kuvihamisha ndani na kufunga baadhi ya vyumba na kufanya mawasiliano kwa ndugu na jamaa.

Nilikuja kuanza kulia siku chache baadae nilipoambiwa nichome moto magazeti yake ambayo alikuwa ananiagiza nimnunulie na kumsomea headlines akidai atayasoma kwa kina akipona. Na nilipoanza kulia hakuna mtu mwingine alikuwa analia.
 
Watu wanatofautiana....
Mama yangu kafiwa na baba yake (walikua karibu mno), mama yake (ukaribu haswa) na mumewe (mpaka alimuuguza kwa muda mfupi aliokuwa hospitali) lakini sikumuona akitoa chozi

Babu na bibi yeye ndo alikua mstari wa mbele kufanya mambo yaende sawa (kwao hamna mtoto wa kiume wa kumpa majukumu)

Ila kuna dada yake alifariki ghafla tu akiwa peke yake sukari ilishuka na hapo ndo nilikiona kilio cha bi mkubwa msibani tena hakulia ile ya kulia ila alimwaga machozi balaa
 
kwani huwa wanalazimishwa kulia??
Context again. Nimesema perception, mtazamo. Kuna wanaolazimisha kwa mtazamo, hata humu nyuzi za kifo cha Mafulu na Dk. Ndugulile wapo wanaolalamika kwanini watoto "ni wakavu" na wanaongea Kingereza, huku mama alionekana anachagua kipande cha kuku.

Wanalazimisha kwa mtazamo, wanatamani mfiwa ajigaragaze azimie ndio aonekane ameumia sana.
 
Kama kawaida yenu baadhi kwenda kwa mkumbo bila kuelewa context.

Mleta mada anahoji perception ya walioenda msibani kulazimisha wafiwa kulia, mleta mada haoji wafiwa kutolia.
asante sana. Wamesoma heading tu wakaanza kutiririka ndio maana maswali yao ni "ulishawahi kufiwa, mara ukifiwa utajua".
 
Context again. Nimesema perception, mtazamo. Kuna wanaolazimisha kwa mtazamo, hata humu nyuzi za kifo cha Mafulu na Dk. Ndugulile wapo wanaolalamika kwanini watoto "ni wakavu" na wanaongea Kingereza, huku mama alionekana anachagua kipande cha kuku.

Wanalazimisha kwa mtazamo, wanatamani mfiwa ajigaragaze azimie ndio aonekane ameumia sana.
Hapa nipo msibani waombolezaji wanalalamika mbona mke wa marehemu halii, mara amepata hadi nguvu ya kupaka lipstick. Mara watoto wa marehemu utadhani hawajadiwa wanakimbizana tu." Ndio nikapata hili wazo la hii mada.
 
Hakuna ulazima...

Ukishajua marehemu kilichomsibu mpaka kupelekea kifo chake unaweza ukacheka sana mpaka kububujikwa na machozi...

Cc: Mahondaw
 
Back
Top Bottom