Kuna ulazima wowote kidini au kimila kulia unapofiwa?

Kuna ulazima wowote kidini au kimila kulia unapofiwa?

Hakuna anatolia kwa ajili ya show off, kulia ni tendo la asili litokanalo na hisia zinazoumiza.

Hivyo hisia hizo za maumivu ndio huamua ulie au ubaki mkavu.

Haulii kuonesha watu.
 
Habari,

Hivi kwani ni lazima mtu kulia hadi uso uchakae unapofiwa na mtu wako wa karibu (wazazi ,mwenza,mtoto, ndugu)? Au ni lazima kulia mbele za watu wajue umelia?

Kwanini watu wakienda kwenye msiba wanataka wakimuona mfiwa wamuone kachakaa, macho yamevimba uso umeumuka kwa ajili ya kulia? Kwani mtu kuhuzunika ni lazima alie? Au kwani kulia ni lazima? wasipolia ndio inaonekana kifo hakijawaumiza? na hata kama kifo hakijawaumiza nyie mnakasirika nini,?

Kuna watu wakisikia tu mtu kafiwa, halafu waone amependeza zake hajachakaa sura, akiona cha kuchekesha anacheka na simu anatumia anaingia mtandaoni wanakasirika hatari, utasikia "umefiwa mara hii tayari upo sawa na mtandaoni unaingia na kucheka unacheka"..mimi naona ni kama kuwaonea wivu wafiwa.

Kila mtu ana namna yake ya kuomboleza, tuache kuwaletea makasiriko wafiwa wanaoweza kuhandle msiba vizuri.
Ulifanikiwa kujua ladha ya chakula Cha msibani bac jua msiba haukuhusu kwaleo ngoja niishie apa
 
Si lazima, nilifiwa na mzee nikakausha kikauzu tu ili nisiwahuzunishe wadogo zangu watano kwa muda ule.
nilikuja kulia peke yangu miaka 20 iliyofuata.
 
Back
Top Bottom