Kuna umuhimu body spray na perfume zisambazwe bure kama kondomu maana kwenye madaladala humu tutakufa

Kuna umuhimu body spray na perfume zisambazwe bure kama kondomu maana kwenye madaladala humu tutakufa

Rorscharch

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
878
Reaction score
2,014
Saa 12 asubuhi, mtu kashuka kitandani, hajafikiria maji wala sabuni, lakini tayari yuko kwenye daladala. Jamani, unajua ananuka kama amegaragara na mwanamke halafu akaamua kwenda moja kwa moja kazini? Hakuna hata sekunde ya kufikiria kuwa wenzako pia wanapumua?

Najua wanaume hatupaswi kufuatiliana, lakini kuna mipaka! Maisha yamekuwa magumu? Sawa. Lakini kuna kile kiwango cha chini kabisa cha kujiheshimu—bare minimum! Usiseme hauna hela, kuna hata vile viperfume vya buku unajipaka, lakini hapana, wewe umeridhika na harufu yako ya kufa mtu.

Bora yangeishia hapa, lakini hapana, kuna wale ambao wamevaa boxer ya wiki nzima bila kufua! Aisee, ukikaa kwenye siti, halafu mtu akashika bomba pembeni yako, unaweza kupatwa na kiwewe kwa mshangao wa kugundua tofauti pekee kati binadamu na beberu ni manyoya! Na hata hilo beberu linaweza kuwa safi zaidi.

Acha uvivu wa kujitunza. Tuache kutesana. Usituletee hewa chafu asubuhi na mapema!
 
Watu wanangangana tu kuish dar maisha magum jua kali dum la maji tu 500 apo anawaza aoge au aifanye naul mana dar uez kutembea hata kilomita 3 kwa mguu.. ndio mana hata wadada unakuta sura safi ila miguu kama katoka kwenye ngoma
 
Hujakutana na daladala zinazotoka ferry 😁😁, hiyo ni cha mtoto maana harufu zote mixer shombo ya samaki lazma ufurahi. Japo binafsi bora hizi harufu kuliko harufu za perfume za buku zinazomwagwa chini, lazma uumwe kichwa maana huwa ni kali zaidi ya udi
 
Nunua barakoa au tembea na zile mask za kuchuja hewa.
Wengine hiyo asubuhi ninyi mnapoenda kazini kina sie ndio tunatoka kazini na sio kutoka kuamka kama wewe.

Acha nikupe pole tu, na kukusihi utuvumilie ama lah ongeza kipato chako huku tuachie sisi.
Kazini kwenu hakuna mabafu unaweza kuoga kabla haujarudi nyumbani
 
Mkuu sasa kama spray au perfume zikisambazwa bure huoni kama ndiyo itakua hatari zaidi. Sababu kila mmoja atakua ananukia harufu yake, sasa patatosha hapo ....??
 
Nunua gari Mzee, maana ya public is for everyone, unajua kwenye public kuna watu wanalala ardhini na wanaona ni sawa?
Public nayo iwe na standard, kama tunaoneana aibu hatutembei uchi kwanini usione aibu kwamba unanuka kama beberu
 
Mkuu sasa kama spray au perfume zikisambazwa bure huoni kama ndiyo itakua hatari zaidi. Sababu kila mmoja atakua ananukia harufu yake, sasa patatosha hapo ....??
Itasaidia kuvutia Nyuki, tutakuwa tunachota asali vituo vya mabasi
 
Public nayo iwe na standard, kama tunaoneana aibu hatutembei uchi kwanini usione aibu kwamba unanuka kama beberu

Who decides public standard? You decide kwa kutafuta mbadala, public sucks, umewahi tumia vyao public vya mahakama nyingi Tanzania? Aibu tupu
 
Back
Top Bottom