Tumeagizwa yote tufanye kwa jina la Yesu, ikiwemo kula,kusafiri,kwa wanandoa hata sex ifanywe kwa jina la Yesu.Yaani kumtanguliza Mungu kwani hicho chakula tumepewa na Mungu hata kama tumekinunua kwa fedha zetu ila Mungu ndie alietupa nguvu za kupata hiyo fedha, lakini pia chakula kinapaswa kutakaswa kwani hatujui kimepitia kwenye njia ipi mpaka tunakipata,kwa uthibitisho zaidi soma hapa;
Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.
1 Wakorintho 10:31
Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.
Wakolosai 3:17