Kuna umuhimu wa kuimarisha vitengo vya habari Serikalini, kelele za tozo ni matokeo ya wananchi kutopata taarifa sahihi

Kuna umuhimu wa kuimarisha vitengo vya habari Serikalini, kelele za tozo ni matokeo ya wananchi kutopata taarifa sahihi

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2013
Posts
2,255
Reaction score
1,565
Taarifa sahihi ndio msingi wa umoja na mshikamano, kama Taifa tunahitaji kila Mtanzania apate taarifa sahihi kutoka katika vyanzo sahihi. Serikalini katika kila wizara, halmashauri au taasisi kuna kitengo cha habari kwa ajili ya kutoa taarifa ya utekelezaji wa mambo kwenye taasisi hizo au wizara hizo.

Kwa sasa kuna utekelezaji wa miradi mbali mbali unaendelea, kwa mfano Utekelezaji wa ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme(JNHP) unaendelea, ujenzi wa SGR unaendelea vizuri, Ujenzi wa daraja la busisi unaendelea, barabara mbali mbali zinaendelea kujengwa kwa kiwango cha lami. Kuna ujenzi wa shule za masomo ya sayansi kwa wasichana kila mkoa zinaendelea, ujenzi wa hospital, vituo vya afya, zahanati, majengo ya utawala, soko, stendi, miradi ya maji kila kona ya Tanzania. Maafisa habari waliopo kwenye wizara, taasisi na halmashauri wanaelezea hii miradi inayoendelea kutekelezwa kwa kiwango gani? Ni namna gani wanawafikia watanzania?Je, wananchi wanajua hii miradi inayotekelezwa?

Serikali kupitia wizara, taasisi na halmashauri iimarishe vitengo vyote vya habari, wana habari wawezeshwe kuendana na wakati ili waweze kuwapa watanzania taarifa sahihi za utekelezaji wa miradi inayoendelea. Haikwezekani Waziri au Rais ndio anajukumu la kuwaambia watanzania utekelezaji wa miradi ya maendeleo wakati maafisa habari wa serikali wapo.

Mh. Nape Nnauye(Mb) Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mh. Innocent Bashungwa(Mb) Waziri OR - TAMISEMI saidieni kuimarisha vitengo vya habari vilivyopo serikalini hasa halmashauri ili viweze kuonyesha mazuri mengi yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita. Leo hii maafisa habari wa zile timu mbili ni maarufu kuliko maafisa habari wengi wa serikali, kuna umuhimu wa kuboresha na kuwezesha vitengo hivi vya habari serikalini.

Haiwezekani iwe Waziri, Katibu Mkuu au Msemaji wa Serikali tu ndio wawe na jukumu la kuelezea utekelezaji wa miradi ya Maendeleo wakati kuna maafisa habari serikalini wenye weledi wa kuweza kuelezea pia. Dunia imehamia kiganjani maafisa habari waje duniani waelezee mazuri yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Wananchi wakipewa taarifa sahihi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, watajua kodi na tozo zinazolipwa kweli zinasimamiwa vizuri katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Watanania lazima tuelewe kodi na tozo tunazolipa ndizo zinazoenda kutekeleza miradi ya maendeleo ili kuweza kuwahudumia Watanzania.

Maafisa habari wetu wasiogope spana za wakosoaji na wale wenye kazi ya kupinga na kutukana bila hoja, wajitokeze kwenye platform tofauti kuelezea mazuri ya serikali.

Hongereni saaa Mh. Mohamed Mchengerwa(Mb) Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo - Gerson Msigwa -Msemaji Mkuu wa Serikali, DK Hassan Abbas - Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye(Mb) Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mh. Innocent Bashungwa (Mb) Waziri OR - TAMISEMI, Mh Hussein Mohamed Bashe(Mb) Waziri wa Kilimo, Mh. Juma H. Aweso(Mb) Waziri wa Maji na mawaziri wengine kwa namna mnavyopambana kufikisha taarifa sahihi licha ya wakati mwingine kukutana na sapana kali au kupata kejeli na matusi kutoka kwa watu ambao kazi yao ni kupinga tu. Hamjawahi choka kumsaidia Mh. Rais Samia Suluh Hassan katika kuwahudumia watanzania, mara nyingi mmekuwa mkitolea ufafanuzi wa mambo mbali mbali kwa kuweka ukweli bayana.

Serikali ya awamu ya sita chini ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kwa mwaka huu wa fedha imetenga jumla ya shilingi bilion 75. 98 kupitia halmashauri zote nchini kwa ajili ya mikopo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, vijana tuchangamkie fursa hii adhimu, fedha hizi zimeshaanza kutolewa katika kila halmashauri.

Mungu ibariki Tanzania,
Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
 
Kelele za tozo ni dalili za kuchokwa kwa walamba asali na tawala zao zilizo madarakani kwa wizi was chaguzi.
 
Labda kikosi cha propaganda, kumpamba na kumsifia mwenyekiti wa chama kikifanya kazi tokea Lumumba.

Hawana taarifa wala ushahidi wa chochote kilichofanyika kutokana na tozo zaidi ya wao kuanza kuchomana kuwa mwenzao anafadhili Singida Big Star mara kaagiza mabasi 60 maana ndio kazi pekee ya tozo inayoonekana yaani ufujaji wa pesa za umma.

Nasikia ikulu nyingine kujengwa Makundu-uchi labda nayo ni kazi ya tozo za wadanganyika
 
Labda kikosi cha propaganda, kumpamba na kumsifia mwenyekiti wa chama kikifanya kazi tokea Lumumba.

Hawana taarifa wala ushahidi wa chochote kilichofanyika kutokana na tozo zaidi ya wao kuanza kuchomana kuwa mwenzao anafadhili Singida Big Star mara kaagiza mabasi 60 maana ndio kazi pekee ya tozo inayoonekana yaani ufujaji wa pesa za umma.

Nasikia ikulu nyingine kujengwa Makundu-uchi labda nayo ni kazi ya tozo za wadanganyika
Mkuu usiamini kila kinachozungumzwa kwenye mitandao, mitandao ni kama jalala unamwagwa uchafu wote MWANDENDEULE
 
Maafisa habari pia wawe wanaeleza jinsi Ma VX yanavyonunuliwa na kutumika. Walipa kodi wana haki ya kujua matumizi maana inaonekana matumizi ndio yanaleta maneno kuliko hizo tozo
 
Kwa uongozi gani huo litatekelezeka?

Huu wa kupeana "kishkaji"?
 
Kwa akili ya kawaidi hii Hali inahitaji kuambiwa ugumu wa maisha na vyombo vya habari kweli?

Kama una familia jaribu kuwauliza hata watoto wako,vinginevyo labda iwe unalelewa kwa shemeji.
 
Kwa akilu ya kawaidi hii Hali inahitaji kuambiwa ugumu wa maisha na vyombo vya habari kweli?

Kama una familia jaribu kuwauliza hata watoto wako,vinginevyo labda iwe unalelewa kwa shemeji.
mdudu hali ya Uchumi kwa sasa ni duniani kote uchumi umeyumba sio Tanzania tu, lakini hii haizui kueleza yale yanayofanywa na Serikali
 
Kwa uongozi gani huo litatekelezeka?

Huu wa kupeana "kishkaji"?
Mkuu Matrix19 mimi ninachojua Tanzania kuna viongozi ambao wamepatikana kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo na wanaendelea kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama walichoombea idhini ya kuwatumikia Watanzania.
 
Maafisa habari pia wawe wanaeleza jinsi Ma VX yanavyonunuliwa na kutumika. Walipa kodi wana haki ya kujua matumizi maana inaonekana matumizi ndio yanaleta maneno kuliko hizo tozo
Ni kweli Wananchi wana haki kujua matumizi ya fedha zao, ndio maana CAG huwa anatoa report ya matumizi ya Serikali Tangawizi
 
Back
Top Bottom