Kuna umuhimu wa kuimarisha vitengo vya habari Serikalini, kelele za tozo ni matokeo ya wananchi kutopata taarifa sahihi

Kuna umuhimu wa kuimarisha vitengo vya habari Serikalini, kelele za tozo ni matokeo ya wananchi kutopata taarifa sahihi

Kelele za tozo ni dalili za kuchokwa kwa walamba asali na tawala zao zilizo madarakani kwa wizi was chaguzi.
Sio kweli brazaj Serikali ya awamu ya Sita inaendelea kuwatumikia Watanzania, duniani kote haiwezekani Wananchi wakawa na mawazo sawa.
 
Mkuu Matrix19 mimi ninachojua Tanzania kuna viongozi ambao wamepatikana kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo na wanaendelea kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama walichoombea idhini ya kuwatumikia Watanzania.
Pole kwa kuamini katika kitu ambacho practice yake haivuki 10%
 
Ni kweli Wananchi wana haki kujua matumizi ya fedha zao, ndio maana CAG huwa anatoa report ya matumizi ya Serikali Tangawizi
Lakini wafujaji huwa wanachukuliwa hatua gani? Mbona wana habari wanakaa kimya kuhusu mambo ya msingi kama hayo kwenye maeneo yao? Kuna mantiki gani kutuelimisha tozo tu na kuacha mambo mengine yanayohalalisha ulipaji wa tozo hizo?
Tunataka maendeleo. Kuna wakati ufujaji wa mali ya umma unakatisha sana tamaa. Ndio maana vilio vimekuwa vingi
 
Mnatuona wananchi hamnazo, ikiwapendeza tuleteeni na tozo ya pumzi
 
Back
Top Bottom