Mkuu Matrix19 mimi ninachojua Tanzania kuna viongozi ambao wamepatikana kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo na wanaendelea kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama walichoombea idhini ya kuwatumikia Watanzania.
Lakini wafujaji huwa wanachukuliwa hatua gani? Mbona wana habari wanakaa kimya kuhusu mambo ya msingi kama hayo kwenye maeneo yao? Kuna mantiki gani kutuelimisha tozo tu na kuacha mambo mengine yanayohalalisha ulipaji wa tozo hizo?
Tunataka maendeleo. Kuna wakati ufujaji wa mali ya umma unakatisha sana tamaa. Ndio maana vilio vimekuwa vingi