Kuna umuhimu wowote wa mabucha yetu Tanzania kuuza nyama pamoja na mifupa?

Kuna umuhimu wowote wa mabucha yetu Tanzania kuuza nyama pamoja na mifupa?

Chendembe

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
444
Reaction score
488
Wanabodi, imekuwa kawaida kwa Bucha zetu nchini kuuza nyama na mifupa yake. Awali walitumia mashoka kupasua mifupa hiyo na sasa misumeno inayoendeshwa na umeme imetamalaki.

Kwa hali ilivyo sasa katika Bucha nyingi, mifupa ni muhimu katika kutengeneza faida kwao na karaha kwa walaji.

Uwa najiulizi, kwanini mifupa iwepo. Na uwa nadhani, kutokana na ubora hafifu wa ng'ombe zetu kupelekea kukosa nya za kutosha.

Kama Kuna umuhimu wa mifupa, Basi Mamlaka husika zisimamie vizuri mizani za Bucha zetu. Na ikibidi, Iwe sheria kutumia mizani za kidigitali.

Au, Iwe sheria kuuza nyama na sio mifupa.
 
Ni Bucha ngapi wanakubali kuuza steki?
Na akikubali kukuuzia juwa ni nyama ya Jana na Juzi mixa na ya Leo kiduchu. Ni majanga.
Kama ambavyo walitii sheria ya kuacha magogo ndivyo ambavyo watatii sheria ya kutouza mifupa ila mkubali kilo kuuziwa 10,000 tu sasa!
 
Kiukweli bucha za kibongo ni magumashi.Yaani ukiwa unapita unaona wametundika nyama nzuri kweli.Kimbembe Sasa unaponunua wanavyokukatia nyama za ajabu ajabu Hadi ukifika maskan unajiuliza ile nyama nzuri niliyoona ni hii kweli.
 
Ni Bucha ngapi wanakubali kuuza steki?
Na akikubali kukuuzia juwa ni nyama ya Jana na Juzi mixa na ya Leo kiduchu. Ni majanga.
Sema uvivu TU wa kibiashara mwenye bucha angeweka bei juu ya steki watu wangenunua mbona supermarket unapata steki tupu bila mfupa wowote na watu wananunua

Kenya bucha nyingi huuza steki TU hasa mabucha ya miji mikubwa hukuti huu ujinga wa kutumia gogo na kuuza nyama mchanganyiko utake usitake lazima uondoke na mifupa na mifupa ndio yaweza kuwa mizito na mingi kuliko nyama
 
Wanabodi, imekuwa kawaida kwa Bucha zetu nchini kuuza nyama na mifupa yake. Awali walitumia mashoka kupasua mifupa hiyo na sasa misumeno inayoendeshwa na umeme imetamalaki.
Kwa hali ilivyo sasa katika Bucha nyingi, mifupa ni muhimu katika kutengeneza faida kwao na karaha kwa walaji.
Uwa najiulizi, kwanini mifupa iwepo. Na uwa nadhani, kutokana na ubora hafifu wa ng'ombe zetu kupelekea kukosa nya za kutosha.

Kama Kuna umuhimu wa mifupa, Basi Mamlaka husika zisimamie vizuri mizani za Bucha zetu. Na ikibidi, Iwe sheria kutumia mizani za kidigitali.
Au, Iwe sheria kuuza nyama na sio mifupa.
Mimi siku zote nasemaga kwamba hakuna mfupa mtamu kwa ng'ombe.

Utakuta mtu anasema "napenda nyama mfupa" unapenda wapi bhana huna hela kama mimi tu.

Mimi nikiwa na 10K bora nikanunue steki yote kuliko kutoa 8K kununua mchanganyiko,maana katika hiyo alfu nane kuna mifupa ya nailipia ambayo nakwenda kuitupa tu.
 
Kiukweli bucha za kibongo ni magumashi.Yaani ukiwa unapita unaona wametundika nyama nzuri kweli.Kimbembe Sasa unaponunua wanavyokukatia nyama za ajabu ajabu Hadi ukifika maskan unajiuliza ile nyama nzuri niliyoona ni hii kweli.
Hadi ukomae nyama nzuri unayoona hawatakuuzia watachukua ya Jana halafu wanakata kiduchu ya leo kutupia kwenye mzani

Wenye Bucha Tanzania kuuona ufalme wa Mungu sio rahisi
 
Pamoja na kufahamu tunagusa watu katika kazi yao, nao watambue wafanyayo Yana hudhi.
Pia, kutotoa kitu sahihi kwa malipo sahihi ni wizi Kama wizi mwingineo.
Mamlaka za vipomo na biashara mtulinde katika hili.
 
Hadi ukomae nyama nzuri unayoona hawatakiuzia watachukua ya Jana halafu wanakata kiduchu ya leo kutupia kwenye mzani

Wenye Bucha Tanzania kuuona ufalme wa Mungu sio rahisi
Yaani sio poa. Sijui ile nyama nzuri anakulaga nani.
 
... wauza nyama hususan wa uswahilini ni wapuuzi sana; mizani za digital wanapiga sana usipokuwa makini; kuna namna wana-set chap inaanzia 150 akitoa mzigo anairudisha 0.00 fasta kwa speed ya mwanga. Inahitaji akili ya ziada kung'amua.

Kati ya makosa makubwa utakayofanya ni kuingia buchani na kuanza kumchekea ukadhani anakujali; akili yako muda wote isiache ku-concentrate kwenye settings za mizani kabla, wakati, na baada ya kupiwa nyama. Ukiona tofauti hakikisha unawaka kweli kweli hata kama mmezoeana vipi na ikibidi nyama ipimwe tena na tena; ni haki yako!

Akina mama wanapigwa sana kama kawaida ya watanzania kukosa ujasiri wa kuhoji hata kwa mambo ya msingi au haki yako.
 
Tatizo mnakwenda buchani kununua kilo moja. Na sio nyama kilo moja.......

Kwenye kilo moja unaweza changanyiwa mifupa na nyama, au mifupa, malapulapu , mifuta na nyama kidogo.

Ila ukienda buchani sema nataka kilo moja ya nyama tupu. Utapewa nyama yako ya ng'ombe safii kabisa bila hata mfupa.
 
Kiukweli bucha za kibongo ni magumashi.Yaani ukiwa unapita unaona wametundika nyama nzuri kweli.Kimbembe Sasa unaponunua wanavyokukatia nyama za ajabu ajabu Hadi ukifika maskan unajiuliza ile nyama nzuri niliyoona ni hii kweli.
Biashara nyingi Bongo bado wanatumia mtindo wa kizamani sana. Wanatakiwa kuwa wabunifu zaidi. Kuna sehemu niliona (siyo Bongo) wao hukata nyama mapande makubwa eg nusu kilo na kuendelea na kuweka kila kipande sehemu yake. Mnunuzi anachagua pande analotaka. Hili la mifupa ni tatizo. Ukitaka kupambana nalo mpaka utumie mbinu za medani eg unakuwa customer wa sehemu moja kwa muda mrefu. Wakishakuzoea utakuwa unapata nyama nzuri.
 
Back
Top Bottom