Pamoja na majibu mazuri ya wachangiaji, binafsi naona mleta uzi ana hoja ya kujibiwa.
Tusii-dilute hoja yake kwa kuendekeza mizaha isiyo na tija ilhali kila mmoja wetu anafahamu uhalisia wa mabucha na baadhi yetu mambo haya yamewakuta walipoenda buchani kutafuta kitoweo cha familia.
Ndugu zangu, bucha za Bongo zina udhaifu wa kuzingatia ubora wa kinachouzwa, badala yake inaangaliwa zaidi kurudisha mtaji na faida zao.
Baadhi ya wauza nyama unakuta wanauza nyama yenye ubora wa chini kwa kisingizio cha 'mchanganyiko'. Mteja anawekewa nyama zisizolika kama vile mafuta au 'malapulapu' ambapo ukifikisha nyumbani inakubidi ukate utupe jalalani. Ukijaribu kuwa makini pale buchani lazima ukosane nao, huruhusiwi kuchagua aina ya nyama.
Hebu tafakari, kwa nini ununue nyama kwa fedha, tena kwa kupimiwa uzani, halafu robo hadi nusu ya uzani ni nyama isiyolika kwa raha (Mifupa, sehemu ngumu, mafuta, milenda n.k ) hadi unaamua kuikata na kuitupa.
Hata kama bei haiwalipi wafanyabiashara wa mabucha, tukubali this is primitive!
Kuna pendekezo nahisi nikilitoa hapa nitagombaniwa na wadau kama mpira wa kona.
Lakini tujitafakari upya, kwenye maisha mambo mawili ya msingi - kupata chakula bora na mavazi ndio namna kuu za kutumia pesa zako na ukazifaidi wewe mwenyewe.
Kama bei ya nyama iliyopo haiwalipi watoa huduma, basi mamlaka husika za Serikali ziangalie ni kwa namna gani wananchi wauziwe kilicho bora kwa bei wanayoimudu.
Kwa vile hii 'category' ya mchanganyiko baadhi ya wafanyabiashara wameigeuza kuwa kumbakumba ya kila aina ya nyama za hovyo; Pendekezo mojawapo ni kuweka nyama kwa viwango (lakini ziwe zile tu zenye hadhi ya kuliwa na binadamu ), Kila mtu achague inayoendana na kipato chake, iandaliwe kistaarabu, ikatwe na kupimwa kabla ili kuepusha kuuza kwa kuzingatia sura ya aliyekuja buchani (mtaani kwetu ukituma mtoto mdogo utalia 🙂 ).
Pia, Serikali ifanye uratibu kuhakikisha nyama zilizo duni sana hata buchani zisifike. Zinaweza kuuzwa kwa wanaotengeneza vyakula vya mifugo na matumizi mengine.
Tujenge jamii iliyostaarabika na inayojijali kwa maisha bora.