Kuna umuhimu wowote wa mabucha yetu Tanzania kuuza nyama pamoja na mifupa?

Ushalewa pilau jazia na mbege ulale
 
Siku moja agiza supu ya nyama yenye mifupa, na siku nyingine agiza supu ya nyama ya stake kisha ulete feedback ya taste zake.
 
Nielekeze bucha yako shekh nami nitoe ushuhuda
 
Wanauza ila bei inakuwa zaidi ya ile ya mixer mifupa.
Hivi kuna sehemu ukitaka steki wanakataa kuuza? Mimi nilidhani uchaguzi ni wa mnunuzi. i.e. ukitaka bila mfupa basi unapata ila bei inakuwa kubwa. BTW nchi zilizoendelea nyama kama ya ng'ombe ina grades zake. Kula ''cut'' ina bei yake na unaweza kukuta minofu kutoka sehemu fulani bei yake ni ghali kweli kweli. Ukifanya hivyo kwenye mabucha ya uswahilini watu wataangua kilio.
 
Hahahaha, hii imenikumbusha niliagiza wali nyama mgahawani nikaletewa nyama ikiwa na mifupa.

Nilimuuliza muuzaji kwanini aniletee wali, nyama na mifupa na Mimi nimeagiza wali nyama. Hakuwa na mengi alinibadilishia akanipa nyama isiyokuwa na mifupa
 
Hapana mkuu. Hata mimi binafsi steki tupu bila mfupa siipendi. Sema mifupa isizidi, iwe kiasi.
 
Mteja atazoea taratibu sasa bucha nyingi hawakubali kuuza steki tupu lazima akutupie na mifupa waweke bei ya steki tupu na mchanganyiko mteja aamue mwenyewe
 
Mzee wenyewe wanakwambia hivi, Ng'ombe hawezi kutembea bila migupa.
 
Mkuu kuna wengine wanapenda mifupa.

Huku nilipo mimi ma butcher yote utakuta bei mbili tofauti kwa kilo; mfano, kilo moja ya nyama yenye mifupa 1000, kilo moja ya nyama bila mifupa 1500. Chaguo lako .

Pole sana, ni changa moto za sikukuu. Sikukuu ikiisha wala hutolalamika umeuziwa mifupa kuliko nyama.

Merry Christmas
 
Umuhimu wa mifupa ni kwaajili ya kutengeneza supu na kupika vyakula kama ndizi Kuna baadhi ya vyakula haipendezi kupikiwa nyama zisizo na mifupa usiwe kilaza
 
Mteja atazoea taratibu sasa bucha nyingi hawakubali kuuza steki tupu lazima akutupie na mifupa waweke bei ya steki tupu na mchanganyiko mteja aamue mwenyewe
Kuna bucha zenye bei ya steki tupu. Nadhani ni chache kwa sababu wateja wake siyo wengi. Mambo mengine yanaendena na maendeleo i.e kipato. Bongo ukianza kuweka grades za ''beef cuts'' kama majuu labda uuze Masaki huko.

 
Nunua steak kwani umelazimishwa kula mifupa? Ila fahamu nyama tamu inakaa karibu na mfupa na Ile bone marrow ndio inafanya nyama iwe tamu unless mwenzetu hujui masuala ya nyama.

But unauzaje nyama bila mfupa so utapata hasara? Labda kama kilo moja utauza elfu 35. Ila kila nyama au sehemu ya mnyama Ina utamu wake.

Kupanga ni kuchagua.
 
Umuhimu wa mifupa ni kwaajili ya kutengeneza supu na kupika vyakula kama ndizi Kuna baadhi ya vyakula haipendezi kupikiwa nyama zisizo na mifupa usiwe kilaza
Haina shida Cha msingi wenye bucha wawe na bei mbili za nyama mchanganyiko na steki tupu sio kuforce
 
Haina shida Cha msingi wenye bucha wawe na bei mbili za nyama mchanganyiko na steki tupu sio kuforce
Kwani unaishi Kijiji gani mzee? Mbona ukitaka steki tupu unapata ni hela yako tu ila kusema mifupa haina faida huo siyo ukweli wengine wanataka nyama kwaajili ya kutengeneza supu, supu inapendeza zaid ikiwa na nyama zenye mifupa pia hata pilau hivyo hivyo , ndizi nayo inapendeza na mifupa, Nyama choma bila mifupa haiwezi kunoga inakua ni mishkaki tu kila kitu kwa ng'ombe kina faida yake.
 
Utakuwa na vinasaba vya Diana Zongo na Chid Benz wewe au mbepo imeanza kazi yake
 
Ni Bucha ngapi wanakubali kuuza steki?
Na akikubali kukuuzia juwa ni nyama ya Jana na Juzi mixa na ya Leo kiduchu. Ni majanga.
Mkuu Morogoro steki elfu 11 na unakatiwa hata kilo kumi. Mchanganyiko na mifupa elfu nane
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…