Kuna uwezakano muumba ulimwengu aliacha kuingilia mambo ya ulimwengu aliouumba?

waisrael walipitia mateso zaidi ya miaka mia4 uko misri ndipo Mungu akaskia kilio chao.
Una uhakika gani alisikia kilio chao na sio kwamba hali ya mambo ya kijamii ilibadilika tu kuwa favourable kwa upande wao huko Misri kama vile utumwa wa Waafrica ulivyokosa mashiko kwa British Empire wakaamua kuachana nao??
 
Kama ni vigumu sana kuamini kwamba ulimwengu umekuwepo au umejitokeza bila muumbaji,

Imekuwaje kwako ni rahisi kuamini muumbaji usiyemjua wala hujawahi kumuona au kumthibitisha yupo, Kwamba ndio muumbaji wa dunia na yupo tu bila kuumbwa?

Kwa nini umu exclude huyo muumbaji kwenye logic ya kuumbwa?

Kama haiwezekani ulimwengu kuwepo tu wenyewe bila kuumbwa, Pia haiwezekani hata huyo muumbaji awepo tu mwenyewe bila kuumbwa.

Na kama si lazima kila kitu kiwe na muumbaji, Hata ulimwengu hauhitaji muumbaji.
Kuna kitu kinaweza kuwa hakina chanzo/muanzilishi/muundaji/muumbaji wake??
 
Yeremia 33 : 5. ....... ... ambao kwa ajili ya uovu wao wote nimeuficha mji huu uso wangu.
 
Kuna kitu kinaweza kuwa hakina chanzo/muanzilishi/muundaji/muumbaji wake??
Inawezekana ndio.

Kama kila kitu lazima kiwe na muumbaji wake,

Je muumbaji wa "muumbaji wa kila kitu" ni nani?

Kama kila kitu lazima kiwe na muumbaji wake, Hata Muumbaji wa kila kitu lazima awe na Muumbaji wake.

Na kama si lazima kila kitu kiwe na muumbaji wake, Basi hata ulimwengu hauhitaji muumbaji wake.
 
Kama ni vigumu sana kuamini kwamba ulimwengu umekuwepo au umejitokeza bila muumbaji,

Imekuwaje kwako ni rahisi kuamini muumbaji usiyemjua wala hujawahi kumuona au kumthibitisha yupo, Kwamba ndio muumbaji wa dunia na yupo tu bila kuumbwa?

Kwa nini umu exclude huyo muumbaji kwenye logic ya kuumbwa?

Kama haiwezekani ulimwengu kuwepo tu wenyewe bila kuumbwa, Pia haiwezekani hata huyo muumbaji awepo tu mwenyewe bila kuumbwa.

Na kama si lazima kila kitu kiwe na muumbaji, Hata ulimwengu hauhitaji muumbaji.
Ili kuepuka mfululizo usio na mwisho wa sababu, lazima kuwe na sababu ya awali ambayo yenyewe haina sababu. Sababu hii ya kwanza ndiyo tunayomwita Mungu. Mungu ni sababu ya kwanza isiyohitaji sababu nyingine yoyote. Uwepo wa Mungu hauhitaji sababu nyingine yoyote kwa kuwa ni wa kujitegemea.
 
Kwani ulimwengu wenyewe hauwezi kuwa hiyo sababu ya awali?

Hata ulimwengu upo wenyewe tu, Na hauhitaji sababu nyingine yeyote ya uwepo wake.

Kwa nini uunde dhana ya kufikirika uiite "Mungu" Halafu huwezi hata kuithibitisha ipo, Kisha uanze kudai ndio sababu ya uwepo wa ulimwengu?

Ulimwengu ulikuwepo, upo na utaendelea kuwepo.

Ulimwengu Hauhitaji sababu nyingine yeyote ile kwa vile wenyewe ndio sababu ya awali.
 
Ndio ulimwengu hauwuwezi kuwa sababu ya awali kwasabu Ulimwengu unajumuisha vitu vyote vinavyobadilika na vinaweza kuacha kuwepo kama binadamu,miti,mawe n.k. Viumbe hivi vinahitaji sababu kwa kuwa uwepo wao si wa lazima.

Mimi na wewe nani mwenye dhana ya kufikirika? wanasayansi wenyewe japokuwa wengi wao hawaamini uwepo wa Mungu Lakini wanahoja juu ya mwanzo wa ulimwengu na mpaka kuwepo kwake wewe unayesema ulimwengu ndio sababu ya awali unayosema hayo ukiwa unafikiria nini?
 
Kila siku hapa duniani kuna habari mbaya za kuteseka kwa binadamu fulani kwa magonjwa, vita, njaa, dhuluma, umaskini n.k kwa viwango tofauti, kuanzia viwango vidogo hadi vikubwa kabisa vya kutisha na kufadhaisha sana

Ni vigumu sana kuelewa kwa nini anayesemwa ana nguvu zote;
Asizue mtoto albino kutekwa, kuuwawa na kukatwa viungo vyake, Asizue watoto kufa vitani Congo, Gaza, Ukraine na kwingine kwingi
Asizue cancer,
Asizuie ubakaji na ulawiti
Asizuie dhuluma za kila aina
Asizue umasikini
Asizue ajali
Asizuie utumwa
Asizuie utapeli wa kidini
Asizuie majanga ya asili

Sasa kwa kuwa ni vigumu sana kuamini ulimwengu ulitokeza au umekuwepo tu bila muumbaji, Je inawezekana muumbaji aliyeuumba ulimwengu aliamua kuuacha ujiendeshe wenyewe tu kwa nguvu na kanuni za asili?

Kwamba aliuumba ulimwengu kisha akaamua kukaa kando kuutazama unavyojiendesha na kujiendea wenyewe tu bila yeye kuingilia kwa namna yoyote au chochote
Mkuu ni hivi. Mungu alimuuamba binadamu kwa mfano wake. Yaani alimpa akili na utashi ili aweze kuendesha maisha yake mwenyewe. Sasa Mungu akiingilia tena haya unayosema huoni kuwa ile principle itakuwa imefutika? Yeye aliachia dunia iendeshwe na binadamu mpaka siku atakaporudi.
 
Ndio ulimwengu hauwuwezi kuwa sababu ya awali kwasabu Ulimwengu unajumuisha vitu vyote vinavyobadilika na vinaweza kuacha kuwepo kama binadamu,miti,mawe n.k. Viumbe hivi vinahitaji sababu kwa kuwa uwepo wao si wa lazima.

Mimi na wewe nani mwenye dhana ya kufikirika? wanasayansi wenyewe japokuwa wengi wao hawaamini uwepo wa Mungu Lakini wanahoja juu ya mwanzo wa ulimwengu na mpaka kuwepo kwake wewe unayesema ulimwengu ndio sababu ya awali unayosema hayo ukiwa unafikiria nini?
Ukisoma sayari zilivyojipanga nakila aina ya nguvu za uvutano utashangaa sana imekuwaje haya yakatokea yenyewe tu?
 
Ndio ulimwengu hauwuwezi kuwa sababu ya awali kwasabu Ulimwengu unajumuisha vitu vyote vinavyobadilika na vinaweza kuacha kuwepo kama binadamu,miti,mawe n.k. Viumbe hivi vinahitaji sababu kwa kuwa uwepo wao si wa lazima.
Kila kitu ni Energy.

Na energy cannot be created or destroyed but can transform from one form to another.

Hivyo si lazima binadamu, miti, mawe viwe vimeumbwa.
Mimi na wewe nani mwenye dhana ya kufikirika? wanasayansi wenyewe japokuwa wengi wao hawaamini uwepo wa Mungu Lakini wanahoja juu ya mwanzo wa ulimwengu na mpaka kuwepo kwake wewe unayesema ulimwengu ndio sababu ya awali unayosema hayo ukiwa unafikiria nini?
Ulimwengu hauna chanzo.

Na hakuna uthibitisho wowote ule wa kisayansi au kidini unaothibitisha kwamba ulimwengu uliumbwa.

Zilizopo ni nadharia tu zisizo na uthibitisho wowote ule zinazo jaribu kuelezea chanzo cha ulimwengu ila hakuna uthibitisho wowote ule.
 
Kila kitu ni Energy.

Na energy cannot be created or destroyed but can transform from one form to another.

Hivyo si lazima binadamu, miti, mawe viwe vimeumbwa.

Ulimwengu hauna chanzo.

Na hakuna uthibitisho wowote ule wa kisayansi au kidini unaothibitisha kwamba ulimwengu uliumbwa.

Zilizopo ni nadharia tu zisizo na uthibitisho wowote ule zinazo jaribu kuelezea chanzo cha ulimwengu ila hakuna uthibitisho wowote ule.
Nishati inaweza kubadilika kutoka hali moja kwenda nyingine, lakini mchakato huu unadhibitiwa na sheria za fizikia. Swali linabaki: Je, sheria hizi zilianzia wapi? Kwa nini sheria hizi zipo na kwa nini zinafanya kazi jinsi zinavyofanya?
 
Kwa nini unadhani hizo sheria zimeanzia sehemu fulani?

Kwa nini hudhani sheria hizi zimekuwepo zenyewe tu?

Vipi je kama sheria hizi zimekuwepo zenyewe tu?

Kama hizi sheria lazima ziwe zimeanzia sehemu fulani, Huoni kwamba hata hiyo sehemu zilipoanzia itahitaji iwe na sehemu nyingine fulani ilipoanzia?

Yani kutakuwa na sehemu nyingi zisizo na mwisho (endless), ili kila sehemu iwe na sehemu ilipoanzia.

Pasiwepo sehemu yeyote ile, iliyo jitokeza yenyewe pasipo kuanzia sehemu fulani.
 
Back
Top Bottom