Kuna uwezakano muumba ulimwengu aliacha kuingilia mambo ya ulimwengu aliouumba?

Unauliza Makofi Polisi
Vyanzo vya Dini ya kiyahudi vinaeleza kuwa Mungu alimpa Ûtawala na Mamlaka Mwanadamu kutawala dunia so Mungu hajihusishi na dunia hii zaidi ya asilimi 10 tuu
a
 
Wewe unafanana na yule mmoja kati ya wale wezi wawili waliosulibishwa msalabani pamoja na Yesu. Alisema Kama wewe Kweli Mwana wa Mungu jiokoe, halafu utuokoe na sisi.
Sasa kosa la yule mwizi no lipi.?😂😂😂
 
Huyo Mungu kama ana nguvu aje hapa mwenyewe ajidhihirishe hizo nguvu zake.

Mnahangaika sana kumwelezea na kumuongelea Mungu mdhaifu ambaye hayupo na wala hajawahi kuwepo kujidhihirisha mwenyewe.
Ajidhihirishe kwako ili apate nini kwako, ili iweje yaani - Ni sawasawa na miaka ya 60's watu vijiji vya ndanindani huko hawajawahi kumuina Nyerere - ingawa wanaskia yupo, wanaona effect za matamko yake mpaka huko chini then waanze kukaza fuvu " huyo Nyerere wenu aje hapa ajidhihirishe kuwa yupo ni Rais kweli - wakati tayari wanapanga mstari kuchukua sababu kwenye maduka ya ujamaa"
Mungu hana sababu ya kujidhihirisha kwako na wala hakulazimishi - wewe ishi tu utakavyo"
 
Nishati inaweza kubadilika kutoka hali moja kwenda nyingine, lakini mchakato huu unadhibitiwa na sheria za fizikia. Swali linabaki: Je, sheria hizi zilianzia wapi? Kwa nini sheria hizi zipo na kwa nini zinafanya kazi jinsi zinavyofanya?
😂😂 Kwani kila kitu lazima kiwe kimeanzia pahali nyie wafia dini mkoje !?
 
Huyo Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.

Mnahangaika sana kumwelezea na kumuongelea huyo Mungu kwa vile hajawahi kuwepo na hayupo kujiongelea mwenyewe na kujidhihirisha mwenyewe kwamba yupo.
 
Huyo Mungu yupo na ataendelea kuwepo, haijalishi akili zinashindwa kumuelezea kiufasaha kadiri ya matamanio ya kibinadamu.
Na nyie mnahangaika sana kukana vitu ambavyo akili zenu zinashindwa kuvitolea majawabu: Ni bora sisi tunaoacha room ya knowledge ya kutaka kujua zaidi kuliko nyinyi mnaofunga akili zenu kwa ku-amini hivyo vichwa vyenu ambavyo hata mkiulizwa vinatanuka kwa micro inch ngapi kwa sekundi hamuwezi kujibu, hamuwezi kujibu hata usingizi ni nini, unatoka wapi na kwa nini tulale n.k vitu vidogo hivi mnashindwa ndo mnataka hizo akili zenu zichakate kitu kisichochakatika??? Mungu yupo...acheni ujuaji na logic za ajabu
 
Kutokujua kitu fulani haimaanishi kwamba ndio kuna Mungu.

Ni ukosefu wako wa maarifa kuhusu kitu hicho ambacho hukijui.

Unahangaika sana kumwelezea huyo Mungu kwa sababu hayupo na hajawahi kuwepo.

Huyo Mungu kama yupo ajitokeze mwenyewe hadharani ajidhihirishe kama ana huo uwezo.
 
Taratibu wataelewa tu
 
Mwanadamu yupo mbali Sana na upeo wa Mungu. Kumweleza mtu ambae haamini Ni sawa na nzi kujua Kama Kuna super nova
 
Kati ya vitu viwili, wema na uwezo, kuna kimojawapo ambacho huyo Mungu hana. Tumhame huyo Mungu wa Israel ili tumtafute yule wetu wa jadi.
 
Mwanadamu yupo mbali Sana na upeo wa Mungu. Kumweleza mtu ambae haamini Ni sawa na nzi kujua Kama Kuna super nova
Huyo Mungu hayupo ndio maana unahangaika kumwelezea.

Huyo Mungu angekuwepo kweli Kusingekuwa hata na haja ya kuhoji uwepo wake.

Huyo Mungu kama yupo ajitokeze hadharani mwenyewe ajidhihirishe kama ana huo uwezo.
 
Ajitokeze kwa Nani? Kwako au!!
 
Ajitokeze mara ngapi wakati hata jinsi unavyoandika humu na kureason, naona kabisa kuna kitu nyuma ya huyu kiumbe - anayewaza hukuhuku na kuhangaika kujua mambo ambayo hataweza yaelewa..
Unlimited capacity ya kuprocess ya hizi bongo haziwezi kuwa justification ya kutokuwepo kwa Mungu.
Kama tu huwezi jibu kwa ufasaha kwa nini wachawi wanaweza pita kwenye kuta, na tusiwaone kwa macho ndo utaelewa Mungu kweli?
MUNGU SIO KITU (kwamba kinachukua space au kinadecay au ni upepo au kina mwisho au kina mahali utakikuta kimekaa kwenye kiti) - Mawazo ya kibinadamu haya - Ni more than huo uanadamu - thus huwezi kumuona kwa haya macho ya nyama but you can feel Him through out your life...
 
Yaani watu Ni wa ajabu sana. Hata vita inayoendelea mashariki ya Kati hakuna hata chembe ya wazo kwamba Ni kwanini inapiganwa kweli.
Kwa mtu makini lazima kujiuliza Mara mbili mbili.
Au hata ilipofikia technology now inaonesha dhahiri inapita mulemule kwenye maandiko
 
Ajitokeze mara ngapi wakati hata jinsi unavyoandika humu na kureason, naona kabisa kuna kitu nyuma ya huyu kiumbe - anayewaza hukuhuku na kuhangaika kujua mambo ambayo hataweza yaelewa..
Hakuna kiumbe yeyote yule aitwaye Mungu au Bibi yake Mungu.

Mungu mmemtunga vichwani mwenu ndio maana hamuwezi kuthibitisha uwepo wake.
Unlimited capacity ya kuprocess ya hizi bongo haziwezi kuwa justification ya kutokuwepo kwa Mungu.
Mungu hayupo na hajawahi kuwepo.
Kama tu huwezi jibu kwa ufasaha kwa nini wachawi wanaweza pita kwenye kuta, na tusiwaone kwa macho ndo utaelewa Mungu kweli?
Hakuna uchawi, Hakuna wachawi.
Kama Mungu sio kitu, Mungu ni nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…