Kwa mujibu wa Takwimu zinazotolewa Sasa na makada, Mawaziri waliopita na watu tofauti Magufuli ndio Raisi aliyekopa fedha nyingi kuliko Rais yoyote Tanzania ingawa kaongoza muda mfupi. Je, fedha zake alifanyia Nini? Takwimu hazidanganyi.
Inasemekana alikopa trilion 29 kwa fedha hizo zilitosha kujenga reli Dar to Kigoma pamoja na bwawa la Mwalimu Nyerere, kununua ndege na chenchi zingebaki tukagawana.
Sababu reli ingegarimu tilion 16, bwawa la nyerere tilion 6. Ukarabati shule kongwe bilion 100 Lakini mpaka Sasa miradi hiyo haijafika kokotee. Je, fedha ziliilipigwa? Au zilienda wapi. Tupate uhalisia.
Mama juzi kachukua Trilion Moja tu. Lakini kila Mtanzania Anaweza kuona kwa macho pale alipo madarasa, shule mpya na zahanati na vituo vya Afya kila kona.
Hapa hatumsimangi Ila tuwe wakweli. Ukisema stendi ya Mbezi na ya dodoma. Takwimu hazidanganyi. Stendi ya mbezi imegharimu bilion 50 tu. Tilion 1 ingejenga stendi Kama hizo 20 tanZania nzima. Sasa t.. 29 alifanyia Nini? Soko la Dodoma na stendi gharama yake NI billion 35 tu. Yani Tillion 1 NI soko na stendi Kama ya dodoma 30.
Na soko na stendi ya Mwanza mradi aliusitisha kabisa mama ndio kaanza nao. Jamani tilion sio mchezo 29 alipeleka wapi? Dalaja la wami NI b 66tu na kaliachs bado. Tilion NI bilion 1000. Faraja la busisi NI billion 600. Hilo ndio nusu tilion. Kifupi ukichukua madaraja. Yote, masoko na stendi alipojenga na kufikia bado haifiki tilion 1. Hizo 28 zilifanya Nini.
Kikwete miaka 10 tilion 20. Kaunganisha kilometa 10,000 za Rami ambazo gharama yake NI Tillion 9 hivi. Yani unaona.
Yeye hajajenga hata km 1000tu za Rami. Sasa hizo tilion 29 tulipigwa?
Mnakjibu mje na takwimu halisi sio ushabiki. Usiwe tulipewa mikopo ya kichina. Unachukua billion 100 unaandikiwa billion 10000.
Bahati Mbaya hizo za kikwete nazo umeonyesha bilion 9 tu kazi ya hizo zote.
Nakupa kazi za Magufuli.
1. Umeme vijiji elfu 9.
2. Ndege mpya 11.
3, Ukarabati shule zote kongwe, unazishaji wa shule mpya.. gharama yake ni zaidi ya hayo madarasa ya samia.
4. Ujenzi wa makazi ya polisi.
5. Flyover - Mfugale na Ubungo-Kijazi.
6. Barabara - Anza na Morogoro road kwa Dar njia nane.. Barabara ya Mbeya hadi Kigoma na Bukoba. Nenda Pale Arusha kwa mara ya kwanza wamejengewa barabara nzuri sana. Itigi -Tabora. Mbeya - Chunya, Songea - Mbambay.
7. Miradi ya maji ndo usiseme.. Nakutajia Miradi Mikubwa tu; Arusha,Mwanga na Same; Mwanza, Mwanza Tabora, Dodoma, Dar, Kisarawe. n.k.
8. Ujenzi na upanuzi wa viwanja vya ndege. KIA, Dar, Songwe, Songea, Chato,Mtwara, Katavi, Iringa, Njombe, Msoma,Mwanza n.k.
9. Kuhamia Dodoma. Makao makuu.
10. Ujenzi wa hostel zax vyuo mbalimbali kama UDSM na TIA (Mtwara Singida na Mwanza).
11. Ujenzi wa Bwawa la Umeme.
12. Ujenzi wa SGR.
13. Ujenzi wa Mwendo kasi ya Mbagala.
14. Ujenzi wa Masoko kila mkoa.
15. Upanuzi wa vituo vya kufulia umeme - Kinyerezi.
16. Ujenzi wa Stend za mabasi kila mkoa.
17. Ujenzi wa Hospital za Kila Kanda.. Kanda ya Kati Dodoma, Kusini - Mtwara. Kanda ya Ziwa Chato. Magaribi - Mbeya.
18. Ujenzi wa Hosipital ya Kila mkoa - Njombe; Msoma n.k.
19 . Ujenzi wa hospital za wilaya.
20. Ujenzi wa vituo vya afya - Kata
21. Ununuzi wa Meli kila ziwa - Victori, Nyasa na Tanganyika.
22. Ujenzi wa Madaraja makubwa -- Busisi na Coco.
24. n.k.
Naishia hapo..hizi kazi zote ndani ya miaka mitano ..Mwanamme alikuwa halali kwa ajiri yako na wajukuu zako.