kama mazungumzo na makubaliano yao yatamalizika vizuri kama yalivyo anza, na wakaafikiana vyema, basi ni wazi mungwana anakwenda kuchukua nafasi muhimu sana ya uongozi wa juu kitaifa ndani ya ACT WAZALENDO...
demokrasia ndani ya vyama vya siasa inashamiri na kusitawi vyema, na kwakweli inazidi kuimarika zaidi nchini 🐒
Mungu Ibariki Tanzania
Naunga mkono hoja mtu yeyote kuwa huru kuhamia chama chochote ndio maana tulitoa ushauri huu kwa Chadema
Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je, tunarejea nchi ya chama kimoja? ila tukubali tukatae wanachama na viongozi hawafanani, kuna wengine ni nguzo na mtaji, hivyo wanategemewa sana, huku wengine ni magarasa tuu.
Magarasa wakihama, hakuna athari zozote lakini nguzo zikihama, zina athari kubwa.
Heche ni nguzo!, kwangu mimi huyu ndiye mtu wa kumpokea Mbowe Uenyekiti, hivyo taarifa za uzushi kama hizi, zinatishitusha!, haswa kwa kuzingatia John Heche ni kutoka kabila la watu wenye msimamo.
Tanzania tuna makabila mengi, kuna makabila walaini laini unawaswaga tuu kama ng'ombe na kuna makabila wagumu wenye misimamo.
Ukisikia mtu wa makabila laini laini amehama hushangai, ila Ukisikia mtu wa kabila gumu amehama chama, lazima ushangae.
John Heche namuaminia, mimi ni Tomaso hii habari siiamini kuwa ni ya kweli mpaka...
P