Kuna uwezekano kuboost Battery ya Gari kunaua Battery iliyo nzima

Kuna uwezekano kuboost Battery ya Gari kunaua Battery iliyo nzima

Nelson Kileo

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2011
Posts
3,053
Reaction score
3,259
Nimenunua Battery mara mbili ndani ya miezi mitatu, zote zimekufa bila taarifa wala kudumu.

Nimechunguza huwa si mchoyo wa kuboost Gari kama nikikutana na mdau aliye na low voltage, jirani yangu mmoja amekua na tabia hiyo almost kila baada ya siku mbili lazima aniombe nimboost.

Jana nawasha Gari mzigo haupigi. Je, hilo la kuboost linaweza kuwa Tatizo kwa Batter zangu zilizokufa au ipo sababu nyingine ya kiufundi.
 
Mkuu kwanza pole, Mimi labda nikuulize maswali kadhaa.

1. Kabla ya hizo battery mbili zilizokufa mambo yalikuwaje? Au ndio umenunua gari na kuanza kukumbana na hizo changamoto?

2. Je kuna siku umewahi kuiacha gari yako kwa muda then ulipokuja kuiwasha ikakugomea mpaka ulipoboost kwa battery nyingine?

Nijibu kwanza hayo tuone shida iko wapi.
 
Tafuta mtaalamu wa umeme. Kuna mahali gari inashida. Mfano mimi, wiki 3 zilizopita nilipata shida ya betri kukosa nguvu mara kwa mara mpk nibust,ila sikuafiki kununua nyingine kwani ndio ina miezi 3 tu....nilifanya utafiti, nikakuta waya wa ethi umekatika mahali,nikaweka mwingine shida ikaisha.
 
Mkuu kwanza pole, Mimi labda nikuulize maswali kadhaa.

1. Kabla ya hizo battery mbili zilizokufa mambo yalikuwaje? Au ndio umenunua gari na kuanza kukumbana na hizo changamoto?

2. Je kuna siku umewahi kuiacha gari yako kwa muda then ulipokuja kuiwasha ikakugomea mpaka ulipoboost kwa battery nyingine?

Nijibu kwanza hayo tuone shida iko wapi.
Ndio
Number 2.
 
Tafuta mtaalamu wa umeme...kuna mahali gari inashida....Mfano mimi,wiki 3 zilizopita nilipata shida ya betri kukosa nguvu mara kwa mara mpk nibust,ila sikuafiki kununua nyingine kwani ndio ina miezi 3 tu....nilifanya utafiti,nikakuta waya wa ethi umekatika mahali,nikaweka mwingine shida ikaisha.
Oooh .
Dah aisee nimetupa N70 ..nikaja nikatupa N70 tena ..sasa now nina N40 nayo chali .. dah
 
Back
Top Bottom